Posts

KAMA KIONGOZI HUFANYI KAZI YA KUMSAIDIA RAIS SAMIA HALAFU UNAIBUKA NA KUSEMA ETI MAKONDA ANAHOJI KAMA NANI, NIWAAMBIE MIMI NDIO MSEMAJI WA CCM SITAFUMBIA MACHO - MAKONDA

Image
SONGWE  "Viongozi wote iwe ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu au Ofisi yoyote ile ndani ya Nchi yetu ya Tanzania yawapasa kufanya kazi kikamilifu, wapo baadhi ya Viongozi wao wanakaa tuu maofisini Dodoma au Dar es salaam na kula viyoyozi tu, fanyeni ziara mkague watendaji wote na muache tabia ya kukombatiana na kufichiana siri" "Tembeeni na sio kusubiria CCM ikija kwenye mikutano hii mnaanza kufunga tai na kuanza kuongea ooh anaongelea sheria kama nani ? nawajibu kuwa Naongelea kama Mtanzania" "CCM tunataka kila Mwananchi ahudumiwe na sio kutishana na mimi sitishiki kabisa mnatakuwa kukumbuka kwamba hata hiyo mishahara mnayopewa ni kodi ya Watanzania" "Mimi ndio msemaji wa CCM na ninasema kwa niaba ya Mwenyekiti wetu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nimeapa nitasema ukweki bila kumung'unya maneno na kama mnadhani nitakufa sasa ..hapana Mungu wetu wa upendo bado ananihapa Afya njema" "Wapo baadhi ya Viongozi wapo Serikalini wanakula vizuri, wan

RAIA AUSTRIA AWEKA REKODI YA KUPANDA KILIMANJARO MARA 150

Image
Raia wa Austria Rudi Stangl (62) mwenye miwani (katikati) akiwa na waongoza watalii mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro kwa mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 . Raia wa Austria Rudi Stangl (62) akiwa njiani kuelekea kilele cha Uhuru Mlima Kilimajaro  Mhifadhi Vitus Mgaya kutoka idara ya Utalii (KINAPA) akimpongeza na kumvisha medali Rudi Stangl mara baada ya kushuka kutoka kilele cha Uhuru alipopanda kwa mara ya 150 .  Na Dixon Busagaga- Kilimanjaro  RAIA wa Austria Rudi Stangl (62) amejiwekea rekodi ya kupanda na kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 ,rekodi aliyoanza kuitafuta tangu mwaka 1982 . Huenda Rudi akawa raia wa kwanza kutoka nchi ya Austria kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kuweka rekodi hii lakini pia kuwa miongobi mwa mawakala wa utalii waliotangaza vyema kivutio cha utalii cha mlima Kiliman

KUTUMBULIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI "HUENDA TATIZO LIMEANZIA HAPA "

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kimekimba . Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kwa vyombo vya habari . Hata hivyo sababu za kutenguliwa kwake hazikuweka wazi ,Tza Media Hub imekusogezea kikao cha hivi karibuni cha kutathimini utendaji kazi kwa Wafanyakazi wa Dawasa ambapo Mhandisi Kimikimba alipata nafasi ya kuzungumza.
Image
  Na Dixon Busagaga ,Ngorongoro. MWANAMKE mmoja aliyepoteza Jicho,Masikio pamoja na Viganja vya mikono yake miwili baada ya kushambuliwa na fisi wakati akinusuru mifugo yake isiliwe katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ameiomba Serikali kumpatia msaada ikiwa ni pamoja na kuhamishwa kutoka katia eneo hilo. Rose Kapande (50) Mkazi waa Kijiji cha Esapai kata ya Nainokanoka wilaya ya Ngorongoro ,mkoani Arusha anasema alifikwa na mkasa huo mwaka 2018 ,fisi huyo   anayetajwa kuwa na kichaa cha Mbwa pia akifanikiwa kuua Ng;ombe wanne . Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro linatajwa kama eneo la Uhifadhi Mseto ,masuala matatu yakifanyika kwa maana ya Uhifadhi ,uendelezaji wa jamii inayoishi katika eneo hili pamoja na utalii wakiruhusiwa binadamu jamii ya wafugaji ,Mifugo ,Ng’ombe,Mbuzi na Kondoo kuishi pamoja na Wanyamapori. Hata hivyo utaratibu huo baadhi ya nyaraka zinaeleza kuwa ulikuwa ni sehemu ya majaribio kuona kama inawezekana ukilenga kutizama uwiano wa mambo matatu kwa ma

EFTA KUONGEZA IDADI YA WATUMIAJI WA TREKTA

Image
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw. Dustan Kyobya akizungumza na wakulima wa wilaya ya Kilombero, na kuwahimiza kutumia zana bora za kilimo ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyokuwa yameandaliwa na taasisi ya EFTA inayojihusisha na utoaji wa mikopo ya mashine za kilimo kwa wakulima. Baadhi ya wakulima wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wakati wa mafunzo hayo. Afisa Masoko na Mauzo wa kampuni ya kilimo ya Hughes ya Jijini Arusha, inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa matrekta aina ya New Holland hapa nchini Bwana Boniface Mollel (Katikati), akitoa maelekezo kuhusu trekta za New Holland TT75, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA Bwana Nicomed Bohay (kulia) wakati wa mafunzo ya siku moja ya kilimo bora kwa wakulima wa wilaya ya Kilombero, wengine katika picha ni Bwana Leonce Malamsha (kushoto) Afisa Uendeshaji Mkuu wa EFTA. Afisa Uendeshaji Mkuu wa EFTA (aliyekaa) Bwana Leonce Malamsha akimsajili mmoja wa washiriki walio

MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAKIWA WAMELEWA WAPEWA ONYO

Image
Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi ARUSHA-TANZANIA Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022 katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani. Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva. Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa dola. SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo mbinu. Sambamba na hilo a