ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA JIMBO LA SAME MASHARIKI

Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango akizungumza na wapiga kura wake kwenye chuo cha VETA Maore Wilaya ya Same.
Moja ya jengo la chuo cha VETA kilichopo katika kijiji Maore-Same Mashariki ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikagua na kujionea ujenzi wake,chuo hicho kinafadhiliwa na Kampuni ya Suzuki ya nchini JAPANI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia
Moja ya shamba la Tangawizi 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo la Same Mashariki,Ndugu Kinana pia alipokea taarifa ya kazi  za chama na taarifa ya Utekelezaji wa ilani.
Wananchi wakishangilia jambo
Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara
Mmoja wa watoto akiwa amebeba kipeperushi cha kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake ndani ya Jimbo la Same Mashariki
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi   Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenyee kijiji cha Ndungu wilayani Same.
 Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela akimuelekeza jambo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana walipokuwa wakielekea kuweka mashada ya maua katika makaburi ya watu 24 waliozikwa katika kijiji cha Mang’a kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki wakati wa maporomoko ya milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka kwenye miamba ya mawe wakati alipokagua ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango akivuka maji katika daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki
Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Nape Nnauye na Mama Anne Kilango Malecela wakiweka mashada ya maua katika makaburi ya watu 24 waliozikwa katika kijiji cha Mang’a kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki wakati wa maporomoko ya milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Nape Nnauye na Mama Anne Kilango Malecela wakisali katika makaburi ya watu 24 waliozikwa katika kijiji cha Mang’a kata ya Goha Same Mashariki ambao walifariki wakati wa maporomoko ya milima kutokana na mvua kubwa ilionyesha mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi n Uenezi Nape Nnauye wakielekea kwenye kiwanda cha Kusindika Tangawizi ,mara baada ya kukagua daraja  kijijini Mang’a kata ya Goha Same Mashariki .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuponda kokoto wakati alipokagua ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba Same Mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAZINDUA KITUO CHA KUTOA MSAADA WA KISHERIA

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO