Posts

Showing posts from November, 2015

RAY MBOYA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA NAFASI YA MEYA MANISPAA YA MOSHI.

Image
Msimamizi wa Uchaguzi wa nafasi ya Meya ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Makabayo akizungumza jambo wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo. Baadhi ya Madiwani walioshiriki zoezi la kumpata Meya wa manispaa ya Moshi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Meya wa Manispaa ya Moshi aliyemaliza muda wake na Mbunge wa sasa wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Hotel ya Umoja. Madiwani wakimsikiliza Mbunge Michael kwa makini . Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema akizungumza katika kikao hicho. Waliokuwa washindani katika nafasi ya kuwania kuteuliwa na Chadema nafasi ya Meya wa manispaa ya Moshi,Francis Shio (kushoto)  akimpongeza Raymond Mboya baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 16 dhidi ya kura 10 za Shio . Madiwani wakimpongeza Ray Mboya baada ya kutangazwa mshindi. Raymond Mboya ambaye pia ni diwani wa kata ya Longuo akiz

PSPF WAANZISHA KAMPENI MPYA YA MTAA KWA MTAA

Image
Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba)  akizungumzana vyombo vya habari kuhusu kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika jijini Dar kushoto ni Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary. Na Mwandishi Wetu Mfuko wa hifadhi za jamii wa pensheni (PSPF) kwa kuwajali watanzania waanzisha kampeni ya mtaa kwa mtaa ili kuweza kuungana na wananchi wa maeneo mbalimbali kwa kuwapa elimu  inayohusu mfuko huo wa pesheni kampeni hizo zimeanzia jijini Dar es salaam kwa kutembelea wilaya zote tatu huku wakipita mitaa mbalimbali ya wilaya hizo. Kampeni hiyo imeanza muda mfupi tu mara baada ya mfuko wa pensheni wa PSPF kuungana kwa kutoa huduma na Mfuko wa afya wa NHIF ambapo wanachama wote walio jiunga na kusajiliwa na mfuko wa PSPF watapata manufaa ya kutibiwa kupitia mfuko huo wa afya  wa NHIF kutokana na kuwa wanachama hai. Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) pia naye aliweza kuungana na maafisa wa PSPF kwa

MSD YAKARABATI JENGO LA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KASI KUBWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK.MAGUFULI

Image
Mafundi wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa. Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo. Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari. Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo. Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati. Na Dotto Mwaibale BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini. Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.

CHAMA CHA WASHIRIKA-WAUGUZI TANZANIA KUKUTANA DESEMBA 12, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZAO

Image
  Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Kinondoni jijini  Dar es Salaam, Omary Mkamba (kulia), akimkabidhi cheti cha Usajili wa Chama cha Ushirika -Wauguzi Tanzania  (Tanna Saccos Ltd) , Mwenyekiti wa chama hicho, Kapteni Adam Leyna katika mkutano uliofanyika hivi karibuni. Mkamba ni mlezi wa chama hicho.   Mwenyekiti wa chama hicho, Kapteni Adam Leyna (katikati), akizungumza na wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mkoani Kagera.  Wanachama wakijadiliana.   Wanachama wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wamevalia fulana rasmi mkoani Kagera Viongozi wa chama hicho na wanachama wakiwa katika picha ya pamoja. Na Dotto Mwaibale CHAMA cha Washirika-Wauguzi  Tanzania (Tanna Saccos Ltd) kinatarajia kujadili mafanikio na changamoto zao  mbalimbali katika mkutano wao mkuu  , utakaofanyika Desemba  12, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,  Mwenyekiti wa Tanna Saccos Ltd, Kapteni Adam  Leyna alisema mkutano  huo ni muh

HAPA KAZI TU” YAWAWEKA SAWA WAFANYAKAZI WA DAWASCO.

Image
 Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.   Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji  Mkuu wao. Na Mwandishi, Maalumu Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu”  unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii. “lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” aliongeza Luhemeja Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususa