Posts

Showing posts from October, 2015

WANA CCM MOSHI MJINI WAMLILIA DAVIS MOSHA,NI BAADA YA KUTANGAZA KUTOGOMBEA UBUNGE TENA.

Image
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura. Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo. Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio. Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge . Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo. Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia. Wengine walitishia kujinyonga mbele yake. Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge. Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zi

NMB MOSHI WATOA POLE KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC.

Image
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB katika matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi wakiwasili katika hosptali ya rufaa ya KCMC . Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kashusho akizungumza jambo na afisa habari wa hospitali ya rufaa ya KCMC Gabriel Chiseo.(Kulia). Afisa Uhusiano wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Moshi mjini waliotembelea hosptalini hapo kutoa zawadi na kuwapa pole wagonjwa. Wafanyakazi wa NMB Moshi wakimsikiliza afisa habari wa KCMC,Gabriel Chiseo (Hayupo pichani). Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawai ya Moshi wakishusha zawadi tayari kugawa kwa wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC. Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kashusho akizungumza lengo la kufika katika hosptali hiyo. Wafanyakazi wa Benki ya NMB,wakiwa wamebeba zawadi tayari kugawa kwa wagonjwa waliolazwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC. Wa