Posts

Showing posts from July, 2015

MAKUNDI 5 YANG'ARA NDANI YA TEMEKE KWENYE USAILI WA KWANZA DANCE 100 % TEMEKE.

Image
Usili wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke. Makundi haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza. Mratibu wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza. Akizungumza baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayot

WAJASILIAMALI 150 WAPATIWA MAFUNZO MOSHI

Image
Baadhi ya Wawezeshaji katika mafunzo yaWajasiliamali 150 yanayofanyika katika chuo cha Ufundi Veta mkoa wa Kilimanjaro. Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo. Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na Kusinin(ESAURP) Prof,Ted Maliyamkono akzungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiliamali  wadogo wa mkoa wa Kilimanjaro yanayofanyika katika chuo cha VETA Moshi. Badhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya siku tano. Mjumbe wa  Bodi ya Taasisi ya fedha ya FSDT ,Erick Masinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Baadhi ya wajasiliamali hao. Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Lembris Kipuyo akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha kurasimisha biashara zo ili wapate mkopo na kukuza Biashara. Prof Maliyamkono akitoa neno la Shukrani. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo,wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo. DC Kipuyo akizungumza na

OBAMA TELLS CAPITAL FM HE'D LIKE TO VISIT MARA ,CLIMB MOUNT KILIMANJARO

Image

KUMBUKUMBU :MWAKA MMOJA WA KIFO CHA MPIGANAJI HENRY LYIMO (kipese)

Image
Baadhi ya waamuzi waliofanya kazi ya Uamuzi na Marehemu Henry Lyimo (KIPESE),Nathan Lazaro na Vitaris wakiwa nyumbani kwao na Marehemu kuhani msiba. Kocha Hamad Haule ambaye amekuwa karibu sana na Marehemu Kipese akijaribu kuweka mambo sawa ili kuhakiksha wanaofika Msibani wanapata sehemu ya kuketi. Wadau wa Michezo wakijadiliana jambo katika Msiba huo. Viongozi wa Machava fc ,Abuu Masudi,(wa kwanza walioketi) ,Mtangazaji wa Moshi fm radio Bahati Nyakiraria na Sembi Hassan Sembi alioketi wakisiliza jambo toka kwa Mwamuzi Thomas Mkombozi (aliyesiamama) Baadhi ya waamuzi wa mchezo wa soka mkoa wa Kilimanjaro. Waombolezaji waliofika katika msiba huo. Baadhi ya wanahabari wakijadiliana jambo. Wanahabari wa kike wao pia walikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika nyumbani kwao na Marehemu. Mratibu wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro Yusuph Mazimu pamoja na Mweka hazina Msaidizi Rodrick Mushi wakiwa buze na simu zao kuhakikisha taar

MAHOJIANO NA CHARLES MAGALI NDANI YA WASHINGTON DMV.

Image
Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

MADAKTARI WA DIASPORA WAKABIDHI MSAADA WA DAWA ZA MAGONJWA YA BINADAMU KWA HOSPTALI YA MNAZI MMOJA

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Jidawi akizungumza na Madaktari Diaspora kutoka Washington walipofika Afisini kwake kwa kujutambulisha ujio wao Zanzibar walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiwa chini ya uenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),wakiwa Zanzibar wametoa huduma ya kucheki waginjwa wa Kisukari na Meno na kutoa Elimu ya Afya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar.    Katibu Mkuu Dr Jidawi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Madaktari hao walipofika Afisini kwake wakiwa na Ujumbe wa Watu 17 wakiwemo Madaktari wa Saratani ya Matiti kwa Kina mama, Kisukari na Meno. Madktari wa Diaspora kutoka Washington wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar walipofika Afisi kwake  Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai wakiwa na wenyeji wao wakifuatilia maongezi na Dr Jidawi wa