Posts

Showing posts from January, 2017

MGODI WA BUZWAGI WALIPA ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

Image
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo. Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.  Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakif u atilia hafla ya kukabidhi h u ndi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimi

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA PILISI,NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSHI.

Image
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa. Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo.. Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao. Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto. Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo. Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea

MADIWANI WA MANISPAA YA MOSHI WAWATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA MAWENZI NA KUWAPA ZAWADI.

Image
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ,Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,wakielekea katika wodi walimolazwa wagonjwa kwa ajili ya kutoa zawadi. Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema na Diwani wa kata ya Kiusa,Stephen Ngasa akikabidhi zawadi ya sabuni ya unga kwa wagonjwa waliolazwa katika Hopstali ya Mawenzi. Diwani wa kata ya Mawenzi,Hawa Mushi akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Diwani wa kata Pasua ,Charles Mkalakala akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wagonjwa katika Hospitali hiyo. Madiwani wakiongojea kuingia katika wodi nyingine

TTCL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI TABORA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI SABA

Image
Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu  Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya  TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora. Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba. Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba. Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Tabora Wasichana wakiwa wamebeba masanduku ya vifaa vya maabara vilivyotolewa msaada