Posts

Showing posts from September, 2016

TRA WAIBUKA VINARA WA UTOAJI TAARIFA KWA UMMA MWAKA 2016

Image
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na wadau wa habari kwenye maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Haki za Kupata Taarifa Septemba 28 KATIKA ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam. Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma. MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016. Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa habari kuhusu vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo

SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

Image
  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.   Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.   Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.   Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo  Semina ikiendelea.   Waandishi wa habari wakichukua mambo kadhaa kwenye semina hiyo.   Wanahabari wakiwa makini katika semina hiyo.  Maswali yakiulizwa.   Taswira meza kuu katika semina hiyo. Picha ya pamoja waandishi wa habari na  maofisa wa SSRA. Na Dotto Mwaibale MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), imewataka Watanzania kuondoa hofu iliyojengeka kwenye jamii kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya kifed

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AAHIDI KUWAINUA WASANII WA FILAMU

Image
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza na makundi ya vijana wajasiriamali na wasanii wa Filamu jijini Arusha.Amesema fani hiyo ni muhimu katika kuhamasisha maendeleo na kujenga mshikamano. Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Rebeca Mongy akizungumza juu ya mipango waliyonayo kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na kulia Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha,Tajiel Mahega. Mkuu wa Idara  ya maendeleo ya jamii Jiji la Arusha,Tajiel Mahega akizungumza katika mkutano huo. Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji na Filamu mkoa wa Arusha(TDFAA)Isack Chalo. Burudani ikiendelea kutolewa na kikundi  cha Sarakasi. Burudani ikiendelea kutolewa na kikundi  cha Sarakasi.

WAFANYABIASHARA WA UTALII WANATANGAZIWA KUSAJILI NA KULIPIA ADA YA LESENI YA MWAKA 2016

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA   MALIASILI NA UTALII   WAFANYABIASHARA WA UTALII KUSAJILI NA KULIPIA ADA YA LESENI YA MWAKA 2016         Wizara ya Maliasili na Utalii inawakumbusha wafanya biashara za utalii wasiokuwa na leseni ya biashara hiyo inayotolewa kwa mujibu wa sheria ya Utalii Na. 29 ya Mwaka 2008 Vifungu Na.10 na 31, kuwa wanatakiwa kusajili na kulipia ada ya leseni kwa mwaka 2016 ifikapo tarehe 31 Oktoba, 2016. Biashara za Utalii husika ni hizi zifuatazo: 1 Kampuni za kusafirisha watalii 10 Vivutio vya kuuza bidhaa za urithi (Cultural heritage centres) 2 Kampuni za uwindaji wa kitalii 11 Wajasiriamali wa utalii wa utamaduni (Cultural tourism enterprises) 3 Wawindaji Bingwa 12 Kampuni za kukodisha vifaa vya utalii 4 Kampuni za kusafirisha watalii kwa ndege 13 Ma

TIGO YAWAKUMBUKA WAHANGA WA TETEMEKO MKOANI KWA KUTOA SARUJI MIFUKO 2424

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu(kushoto) akipokea sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu(kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya alipomkabidhi sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni ,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera,wa pili kulia ni Meneja wa Tigo Mkoani humo Sadock Phares. Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya akizungumza na  waanidishi wa habari mkoani Kagera alipomkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu     sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni ,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

MRADI WA URASIMISHAJI ARDHI UBUNGO WAINGIA MIZENGWE WATENDAJI WATISHIA KOGOMA KWA KUKOSA POSHO

Image
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi Na Dotto Mwaibale WATENDAJI na vibarua wanaofanya kazi ya kupima ardhi katika mradi wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela katika Kata ya Kimara  wilayani Ubungo umeingia mdudu baada ya kutishia kugoma kutokana na kutolipwa fedha za posho ya kazi hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu. Hatua hiyo imefikiwa baana ya kuona baadhi ya vongozi wanaosimamia mradi huo wa kuanza kujinufaisha wenyewe na kuwanyonya watendaji wakiwemo vibarua  hao. Wafanyakazi wa upimaji wa ardhi kutoka wizarani na vibarua hao wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili kwa masharti ya kuto andikwa majina yao gazetini  wamesema  viongozi hao kupitia mradi huo wamejenga mazingira ya  kujinufaisha kupitia fedha zilizotoka Benki ya Dunia kufanya mradi huo. "Tunachangamoto kubwa ya kupata fedha za malipo kwa kazi tunayoifanya tumefanya kazi miezi minne lakini tumelipwa mwezi mmoja tu na si sisi peke yetu na hata  watendaji wa wizara wanaofanya kaz