Posts

Showing posts from July, 2017

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROF JUMANNE MAGHEMBE AWATAKA WANAHABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KUTANGAZ VIVUTIO VYA UTALII.

Image
Wahariri na Wanahabari wametakiwa kuendelea kutumia kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali ya Uhifadhi na utalii wa Tanzania ili kutangaza nchi sambamba na kuchangia katika kuukuza uchumi wa Taifa Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni   'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.   .  Prof Maghembe amesema katika kufanikisha kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutegemea utalii Wanahabari wanapaswa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi kwa Watanzania na wageni kwa kutumia kalamu zao. "Nyinyi waandishi wa habari msikubali kuandika jambo ambalo hamlijui kitaaluma, kwani ukifanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo"amesema Prof. Maghembe. Nae Mkurug