Posts

Showing posts from August, 2016

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua   litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi. Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua lin

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA

Image
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na  Paroko wa  Parokia ya Mtakatifu  Petro  Fr.  Stephano  Kaombwe  wakati akiwasili kuhudhuria  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam.  "Maharusi"   Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiingia kanisani  tayari kwa   Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam  "Maharusi"   Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiingia kanisani  tayari kwa   Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam   Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiwa ta yari kwa   Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam    Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  na wageni waalikwa akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufu