Posts

Showing posts from August, 2023

KUTUMBULIWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI "HUENDA TATIZO LIMEANZIA HAPA "

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kimekimba . Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu kwa vyombo vya habari . Hata hivyo sababu za kutenguliwa kwake hazikuweka wazi ,Tza Media Hub imekusogezea kikao cha hivi karibuni cha kutathimini utendaji kazi kwa Wafanyakazi wa Dawasa ambapo Mhandisi Kimikimba alipata nafasi ya kuzungumza.
Image
  Na Dixon Busagaga ,Ngorongoro. MWANAMKE mmoja aliyepoteza Jicho,Masikio pamoja na Viganja vya mikono yake miwili baada ya kushambuliwa na fisi wakati akinusuru mifugo yake isiliwe katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ameiomba Serikali kumpatia msaada ikiwa ni pamoja na kuhamishwa kutoka katia eneo hilo. Rose Kapande (50) Mkazi waa Kijiji cha Esapai kata ya Nainokanoka wilaya ya Ngorongoro ,mkoani Arusha anasema alifikwa na mkasa huo mwaka 2018 ,fisi huyo   anayetajwa kuwa na kichaa cha Mbwa pia akifanikiwa kuua Ng;ombe wanne . Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro linatajwa kama eneo la Uhifadhi Mseto ,masuala matatu yakifanyika kwa maana ya Uhifadhi ,uendelezaji wa jamii inayoishi katika eneo hili pamoja na utalii wakiruhusiwa binadamu jamii ya wafugaji ,Mifugo ,Ng’ombe,Mbuzi na Kondoo kuishi pamoja na Wanyamapori. Hata hivyo utaratibu huo baadhi ya nyaraka zinaeleza kuwa ulikuwa ni sehemu ya majaribio kuona kama inawezekana ukilenga kutizama uwiano wa mambo matatu kwa ma