Posts

Showing posts from December, 2015

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK

Image
Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania   kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania. Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza  kutumia  Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.  Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za  kampuni. Hivi karibuni, Tigo Tanzania imejishindia   tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua mashirikana watu bina

UBADHIRIFU WA FEDHA NA RASILIMALI WAPUNGUA VIJIJINI KWA VIONGOZI KUHOFIA KUCHUKULIWA HATUA NA WAKAZI WA MAENEO HAYO.

Image
  Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda. Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.   Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye si   kiongozi na ni jukumu la wanakijiji wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja mkizithi

Tigo Pesa Yatowa Elimu kwa Mawakala Wao Zenzibar

Image
Mkurugenzi  wa Tigo Pesa Tito Magesho akizungumza na mawakala wa Tigo Pesa walioko Zanzibar wakati wa mkutano wa kuwakutanisha mawakala wa Zanzibar jinsi ya  kuendesha huduma hiyo kwa wateja wao mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari ya ben bella Zanzibar Mawakala wa Tigo Pesa Zanzibar wakipata mael ezo kutoka kwa mmoja wa Maofisa wa Tigo Pesa baada ya mkutano wao wa kutowa elimu ya uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya BenBella Zenj. Msimamizi wa Tigo Pesa Kanada ya Zanzibar Mubaraka akibadilishama mawazo na Mkurugenzi  wa Tigo Pesa Tito Magesho, baada ya mkutano wao na Mawakala wa Tigo Pesa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Ben Bella Zanzibar.  Mkurugenzi  wa Tigo Pesa Tito Magesho akizungumza na mawakala wa Tigo Pesa walioko Zanzibar wakati wa mkutano wa kuwakutanisha mawakala wa Zanzibar jinsi ya  kuendesha huduma hiyo kwa wateja wao mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari ya ben bella Zanzibar

Afya ya Uti wa Mgongo ni Afya ya Mgongo - Dk. Yash Gulati, Apollo Hospital

Image
Dr Yash Gulati, Senior Spine and Joint Replacement Surgeon at Apollo Hospitals; Delhi Na Mwandishi Wetu, Maendeleo katika njia za ufanyaji kazi pamoja na matumizi ya teknolojia yanavyokuwa kwa kasi yanaweza kutufanya tuamini tumepunguza maumivu katika viungo vyetu vya mwili ila si hivyo. Tunatumia magari, mitandao mbalimbali ambayo vizazi vilivyopita havijawahi kuota kutumia. Mabadiliko haya mapya katika maisha yetu yenye msisitizo mdogo katika uimarishaji wa viungo umechukua hatamu na kuathiri maisha yetu kwa maana mwili wa binadamu ni ule ule toka miaka milioni iliyopita. Na hiyo inasababisha kuongeza matukio mengi ya maumivu ya mgongo kwa sababu uti wa mgongo umekwisha athirika. Watu wengi lazima wakutwe na maumivu ya uti wa mgongo walau mara moja katika vipindi vya maisha yao. Sehemu kubwa inayoathirika katika uti wa mgongo ni sehemu ya chini kabisa na sehemu ya shingoni kwa sababu sehemu hizo ndizo zina beba uzito mkubwa wa mwili kila siku. Sababu nyingine zinazo

WANANCHI WA KIJIJI CHA SHENDA WILAYANI GEITA WALALAMIKIA UCHAFU ULIOTUPWA TAREHE 9 DISEMBA

Image
Huo ndio uchafu uliotupwa katika kijiji cha shenda siku ya tarehe 9 Disemba ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima  Wanakijiji wa kijiji cha Shenda wilayani Geita wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho ambapo walilalamikia  kutupwa kwa takataka katika kijiji hicho siku ya tarehe 9 ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima Krantz Mwantepele,Geita Wananchi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9 Lililofanyika nchi nzima.   Wakiongea na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutupa takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.   Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu

RIDHIWANI KIKWETE ATETA NA KATIBU MKUU KIONGOZI,OMBENI SEFUE IKULU

Image
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya Rais Dk John Magufuli kuwaapisha mawaziri waliokuwa wamesalia Ikulu, Dar es Salaam jana.  Ridhiwani pia alipata wasaa wa kujadiliana mambo mbalimbali na kiongozi huyo wa watumishi wa serikali. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Tigo yagawa simu 200 kwenye “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” Rufiji

Image
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na kushoto kwake ni   Dkt. Flora Myamba Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA. Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa k

VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI WAFURAHIA MAFUNZO YA URAGHABISHI

Image
Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya uraghabishi  yaliyofanyika wilayani hapo Na Krantz Mwantepele “Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,”  Hayo ni maneno ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Loliondo, mwezi Agosti  mwaka huu. Alisema hayo kwa lengo la kufafanua dhana ya uwajibikaji kwa viongozi kama njia muhimu ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini katika wilaya yake. Ni dhahiri kwamba viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maeneo husika.  Kuna nafuu kwa watendaji wa kata na vijiji,  ambao ni

WAWEKEZAJI KATIKA MIGODI TANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAKAZI WAISHIO MAENEO HAYO ILI KUPUNGUZA MIGOGORO.

Image
Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo. Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.   Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini.   Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo. Mgodi huo unazungukwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mwendakulima, Mwime na Chapurwa.   La

WATOTO WA WAHADHIRI WA UDSM WAJUMUIKA PAMOJA KWENYE 'GET TOGETHER' YA NGUVU

Image
Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu. Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo. Hakika ilikuwa ni siku ya furaha maana watu walikuwa wanakumbushana mambo ya miaka ya 90 kwani kipindi hicho walikuwa wadogo. Watoto wakiendelea kucheza wakati wa party ya watoto walioishi chuoni hapo kipindi wazazi wao bado ni waalimu katika chuo cha UDSM Full Happy kwa kila tu aliyefika katika Party hiyo. Watoto wa wahadhiri wa UDSM wakibadilishana mawazo kwenye party ya kuwaunganisha pamoja kama wanafamilia wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hakika watoto walikuwa waki-en