Posts

Showing posts from April, 2015

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/

Image
  Asilimia 94 ya madini katika sarafu ya sh. 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello.  Pia ndivyo ilivyoelezwa wakati wa uzinduzi wa sarafu hii mnamo mwezi Septemba mwaka jana kabla haijaingizwa katika mzunguko mwezi Oktoba 2014.  Bw. Kobello amesema hadi sasa sarafu zenye thamani ya sh. 1,162,000,000/- zimekwishasambazwa kote nchini na kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu hiyo endapo itahitajika. “Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya sh. 500,” amesema Bw. Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi. “Kwa hiyo, tunapenda kuwafahamisha wananchi kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu za sh. 500 nchini na kwamba kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake ni kujiingizia hasara,” ameeleza mkurugenzi huyo. Pia ameongeza kuwa Nickel sio miongoni mwa mad

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU KIJIJINI KISANGA.

Image
 Mgeni Rasmi katika Sherehe za uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.   Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akiongea na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama  Shujaa wa Chakula Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kw

ACACIA YAZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE 510

Image
Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, wakimshangilia Meneja Mkee wa mgodi huo, baada ya kumpatia zawadi ya Meneja bora wa mwaka ambaye wao wenyewe wafanyakazi walimteua. Katika hatua  nyinghine, kampuni ya Acacia imewazawadia saruji na mabati wafanyakazi wake 510 wanaofanyakazi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu 500 kwa kuhudumu kwa muda mrefu na 10 kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya kampuni hiyo ya tabia sita (Six Desired Behaviors). Utoaji wa zawadi hizo ulifanyika wakati wa sherehe za siku ya wafanyakazi duniani kwa wafanyakazi wa mgodi huo, Jumanne usiku Aprili 28, 2015. Sherehe za Mei Mosi zitafanyika kitaifa mkoani Mwanza Michell akipongezwa na baadhi ya wafanyakazi   KAMPUNI ya uchimbaji madini, Acacia, imewazawadia wafanyakazi wake wa muda mrefu 500 na wengine 10 kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juuu kwenye mgodi wake wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga. Akikabidhi zawadi h

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

Image
Balozi Amina Salum Ali Na mwandishi wako, Washington, DC Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela. Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya

WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU PATANDI WAZUIA BARABARA YA ARUSHA MOSHI KWA SAA MBILI

Image
Hali ya Sintofahamu imeukumba mji wa Tengeru leo Asubuhi baada ya wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi Kufunga barabara kwa muda wa masaa mawili na kuacha shughuli za maendeleo kusimama kwa muda huku magari  ya abiria yanayokwenda katika mikoa ya Kilimanjaro,Tanga na Dar es salaam na mji mdogo wa usa river na maeneo mengine kupata adha hiyo. Wanafunzi hao walizuia bara bara hiyo  wakishinikiza madai yao kusikiliza kwani wameshatoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo hicho bila ya kushughulikiwa kwa muda sasa wakiainisha kuwa wamekuwa wakipatiwa adhabu zisizo stahiki ikiwemo kurushwa kichura kuchapwa makofi huku kanuni za utumishi zikivunjwa na uongozi wa chuo hicho cha ualimu Patandi kilichopo wilayani Meru.. Wakizungumza kwa nyakati Tofauti na  libeneke la kaskazin i  blog  Mmoja wa wanafunzi  Jenny Mlay  alisema kuwa leo Asubuhi mkuu wa chuo alimkuta mwanafunzi mwenzao amelala bwenini akiumwa na kuacha taa ikiwa inawaka na ndipo alimpiga makofi na wao kwa umoja wao wakaamua

NDESAMBURO NA MEYA JAFARY MICHAEL WASHAMBULIA JIMBO LA MOSHI KWA MIKUTANO.

Image
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika jirani na Super Market ya Nakumat. Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo wakimsikiliza Ndesamburo. Ndesamburo akizungumza. Baadhi ya viongozi wa Chadema akiwemo mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakimsilikiza Ndesamburo. Msatahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara . Mbunge waMoshi mjini Philemoni Ndesamburo akimsikiliza Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi.(hayuko pichani) akiwa na viongozi wengine wa Chadema. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.

MASHINDANO YA LUCY OWENYA CUP YAZINDULIWA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI.

Image
Mbunge wa viti Maalumumkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akiwasili katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Moshi vijijini na kushirikisha kata 16 za jimbo hilo. Baadhi ya wananchi waliohudhulia ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. Mbunge Owenya akicheza ngoma katika shrehe za ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup. Baadhi ya timu zinazoshiriki mashindano hayo zikiwakatika uwanja wa shule ya sekondari Singhiti kwa ajili ya uunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. Mratibu wa mashindano hayo,Charles Mchau akizungumza jambo katika ufunguzi wa mashindano hayo. Mbunge wa Vitimaalumu mkoa wa Kilimanjaro ,Lucy Owenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015 ,Mashindano yaliyoanza katika jimbo la Moshi vijijini yakishirikisha kata za Jimbo hilo. Mbunge wa Viti Maalum Lucy Owenya akisalimianana mwamuzi Batista Mihaf