Posts

Showing posts from May, 2014

Tizama:GARI ILIVYOGONGA TRENI ENEO LA KILOLENI TABORA.

Image
Ajali iliyotokea May 30 ,2014 majira ya jioni maeneo ya Kiloleni mkoani Tabora, ajali ilihusisha Treni (Gari moshi) na gari ndogo iliyopondeka hapo pichani, ndani ya gari alikuwemo mtu mmoja ambaye vyanzo vinaeleza kuwa dereva wa gari ndogo alikimbizwa hospitali na amevunjika miguu. Baadhi ya wananchi wakishuhudia yaliyojiri eneo la tukio

MTOTO NASRA ALIYEKUWA AKIISHI KWENYE BOX AFARIKI DUNIA HOSPTALI YA MUHIMBILI.

Image
MTOTO Nasra aliyekuwa akiishi kwenye.box kwa miaka.minne akidaiwa kuteswa na mamake mkubwa baada ya mama yake kufariki,huku akikosa uangalizi wa karibu,chakula,tiba na huduma.nyingine muhimu AFARIKI DUNIA MUHIMBILI usiku wa kuamkia leo.majira ya saa saba.tatizo ni Nimonia na homa ilipanda sana. R.I.P NASRA wewe mbele.sisi nyuma tutakufuata.Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi

TANAPA YAWATUNUKU VYETI WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI WALIOSHIRIKI KONGAMANO JIJINI MWANZA.

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Raia Mwema na RAIA Tanzania kanda ya kaskazini Paul Sarwat ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA. Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la The East African Adam Ihucha ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA. Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mhariri wa Gazeti la Nipashe Beatrice Bandawe,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa ha

WASHINDI "TANAPA MEDIA AWARDS 2013 "WAPATIKANA.

Image
Mshereheshaji Sauda Simba Kilumanga akiwakaribisha wageni katika ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe za utolewaji wa Tuzo kwa Wanahabari zinazoandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA)Paschal Shelutete akifanya utamburisho wa wageni mbalimbali waliofika katika shughuli hiyo. Baadhi ya wageni mbalimbali katika shughuli hiyo. Meza kuu iliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Lazaro Nyarandu. Waziri Nyarandu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA,Ibrahim Mussa. Mmoja kati ya wageni waalikwa alikuwa ni Mkurugenzi wa Umoja wa vilabu vya Waandishi wa Habari nchini ,Abubakar Karsan ambaye alipata nafasi ya kuzungumza machache. Kiongozi wa Majaji waliofanya kazi ya kupitia kazi za Waaandishi walioshindanishwa na kisha kupatikana washindi Dk Ayoub Rioba akizungumza namna washindi walivyopatikana na baadae kuwatambulisha Majaji wenzake. Majaji walioshi