WATANO WASHIKILIWA KWA UJAMBAZI KILIMANJARO







Na Dixon Busagaga,Moshi.
POLISI mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kunasa mtandao wa watu
wanaodaiwa kujihusisha katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi na
uporaji wa kutumia silaha za moto ya hivi karibuni baada ya kumkamata
mtuhumiwa mwingine na kufanya idadi yao kufikia watano sasa.

Mbali na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo pia polisi wamefanikiwa kukamata
bastola aina ya Browning yenye namba 0663 TZ CAR 75516 pamoja na
risasi moja ya bastolailiyotambuliwa kuwa ni mali ya Evance
Masuki(54)mkazi wa Majengo mjini Moshi iliyoporwa na watuhumiwa hao
October 12 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robrty Boaz alisema katika
uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa ,watu hao
walikubalia kuonyesha silaha hizo pamoja na risasi tatu za Shortgun
ambayo inadaiwa kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara wa mbao mjini
hapa Nickson Mushi.

“Katika hatua za uchunguzi tumebaini kuwepo uhusiano na ushiriki wa
silaha aina ya shortgun katika mauaji ya mfanyabiashara Nickson Mushi
aliyeuawa huko maili sita Novemba tisa mwaka huu ambayo tunaifanyia
uchunguzi wa kitaalamu.”alisema Boaz.

Boaz alisema pia wamefanikiwa kukamata komputa mpakato nyingine aina
ya Toshiba ambayo iliibwa hivi karibuni toka kwenye duka liitwalo
Pendeza mini super market mali ya William Mwacha mkazi wa mjini Moshi.

Kamanda Boaz aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na
Emanuel Makala(280 maarufu kama Rama,Seif Hussein(42)maarufu kama
Mwamba ,Eben Mwaipopo(22)maarufu kama Hashimu,Nicolaus Urio(28) na
Emmanuel Kiula(28) wote wakazi wa Moshi.

Boaz alitoa wito kwa wananchi waendelee kiimarisha vikundi vya ulinzi
katika maeneo yao pamoja na kuwa wepesi wa kutoa taarifa za siri za
aharifu na uharifu kwa jeshi la polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa
mapema kabla ya madahara kutokea.

Katika siku za karibuni katika mji wa Moshi na mikoa ya jirani
kumekuwa na matukio kadha wa kadha ya unyang’anyi na uharifu wa
kutumia silaha ambapo miongoni mwa vitu ambavyo vimekuwa vikiporwa ni
pamoja na Laptop,Simu pamoja na fedha.

Juzi kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa, Koika Moita, aliwaambia
waandishi wa habari baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa watuhumiwa hao wa
ujambazi ni pamoja na gari aina ya Toyota Mark II yenye namba T 564
AUW ambalo linaaminika kutumika katika kufanyia uharifu.

Vitu vingine ambavyo walikutwa navyo watuhumiwa hao mbali na bunduki
aina ya Shrtgun pia walikutwa na laptop mbili aina ya Dell na Hp
ambazo  taarifa zinasema ziliporwa katika moja ya maduka yaliyopo
jengo la Kibo tower mjini hapa.

Watuhumiwa hao pia walikutwa na vibao vitatu vya namba za gari (Plate
number) ambazo ni T916 ARK,vibao viwili na T885 AZW ambavyo vinadaiwa
kutumika mara wafanyapo tukio la uharifu kwa lengo la kujificha
kunaswa na askari.

Pia watu hao walikutwa na funguo mbalimbali za magari,Simu nane za
aina mbalimbali ,vocha za mitandao mbalimbali ya simu ambazo thamani
yake haikuweza kufahamika mara moja pamoja na vifaa mbalimba
vinavyoaminika kutumika katika  kuvunjia vikiwemo bisibisi
,Nyundo,Prize  pamoja na Tindo .

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO