EXTRA BONGO KUPAGAWISHA MKESHA KILI MARATHONI.




George Kavishe

Moshi.

WASANII mbalimbali wanatarajia kutoa burudani kesho usiku katika Ukumbi wa Voda House mjini Moshi ikiwa ni mkesha kabla ya kufanyika kwa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon Jumapili zitakazoanzia katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika.



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema jijini Dar es Salaam jana kuwaburudani hiyo ni moja ya hamasa kabla ya kufanyika kwa mbio hizo.

Aliwataja wasani watakaotoa burudani katika siku ya mkesha huo wa Kilimanjaro Marathon kuwa ni Jambo Squad,
Jambo squad









 The Warriors.
 
The warrios









Extra Bongo.
Xtra Bongo

 








Joh Makini
“Kwa mwaka huu tumeona tufanye tofauti kwa kuweka burudani katika siku ya mkesha kabla ya kufanyika Kilimanjaro Marathon,” alisema.

Alisema pia siku ya mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon kutakuwepo na burudani kutoka kwa Joh Makini, Jambo Squad, Wakali Dancers na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma.

Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.

  






Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO