SHAHIDI KESI YA KUSAFIRISHA TWIGA AMKAANGA MTUHUMIWA .
![]() |
| Aina ya ndege inayodaiwa kutumika kurosha wanyama Hai. |
SHAHIDI wa 20 katika kesi ya utoroshaji wanyama hai kwenda Uarabuni ameileza mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi kuwa mshtakiwa wa kwanza
katika kesi ya utoroshaji Twiga kwenda Uarabuni,Kamran Ahmed alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwepo siku ya tukio la kusafirisha wanyama hao.
Shahidi huyo Robert Nyanda mkazi wa Dar es salaam aliieza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa huyo alikuwa ameambatana na watu wengine ambao kwa pamoja walikwenda na gari ndogo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA).
Akiongozwa na wakili wa serikali,Evetha Mushi,mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Simon Kobelo, shahidi huyo mtumishi wa kampuni ya Swissport uwanja wa ndege wa Mwl Julius Nyerere(JKNIA) alieleza
kumuona mshitakiwa uwanjani hapo akiwa na wenzake.
Aliieleza mahakama kuwa mshtakiwa huyo akiwa na wenzake ambao aliwataja kwa majina ya Msakamali na Kimath wafika uwanjani hapo na gari dogo huku gari jingine aina ya Fuso likiwa na wanyama hao tayari
likiwa jirani kabisa na Ndege.
"Wakati natoka ofisini kwangu usiku nikakuta gari aina ya Fuso limepaki tayari karibu na ndege likiwa na wanyama pamoja na timu kubwa ya watu ambao walikuwa na lengo la kusaidia upakiwaji wa mizigo hiyo
katika ndege."alieleza Nyanda.
"Baadae lilikuja gari nyingine ikiwa na Crane(chombo cha kuinulia vitu vizito)maalumu kwa ajili ya kushushia mizigo ilikuja pia gari ndogo ambayo pia ilikuwa na watu wengine,nilimuona Msakamali(aliyemtaja kama mfanyakazi wa TRA)Kimath(ambaye ni miongoni mwa washitakiwa)na watu wengine wawili wenye asili ya Kihindi(Asia)"aliongeza Nyanda.
Alieleza akiwa kama afisa wa kampuni ya Swissport, alikuwa na jukumu la kusimamia,kupakia na kupakua mizigo kutoka katika ndege na kwamba siku hiyo alikuwa ameagizwa na bosi wake aliyemtaja kwa jina la Rosemary Israel, kuandaa vifaa vya aina tatu vya kubebea vitu vizito.
Alieleza mahakama hiyo kuwa siku ya tukio pia alimuona msimamizi wa kitengo cha wanyama katika uwanja huo lakini hakutilia shaka kwa kuwa alijua yupo kazini.
"Kazi ya upakiaji wa mizigo katika ndege ya Qatar ilifanyka majira ya saa nane usiku, sisi hatukuwa na jukumu la kukagua kwa vile ndege haikuwa ya kwetu,tulichotakiwa kufanya ni kusaidia upakiaji wa mizigo
tu,masuala mengine yalikuwa chini ya kampuni ya Equity aviation.
Akijibu maswali ya wakili wa utetezi, Edmund Ngemela, aliyetaka kufahamu alipo bosi wa shahidi huyo,Rosemary Israel, shahidi huyo alisema hiyo haikuwa kazi yake.
Aidha wakili huyo alitaka kufahamu sababu za shahidi huyo kutokagua nyaraka za mzigo uliokuwa ukipakiwa katika ndege hiyo shahidi huyo alisema lilikuwa jukumu la kampuni ya Uquity kwani wao waliombwa kutoa vifaa vya kunyanyua vitu vizito tu.
Naye shahidi wa 21 katika kesi hiyo,Rewald Amani aliyekuwa meneja muongozaji wa ndege katka uwanja wa Kia,alithibitisha kutua kwa ndege hiyo Novemba 24, 2010 katika kiwanja hicho na kuondoka Novemba 26, 2010 ikiwa salama kuelekea Doha Qutary.
Alieleza mahakama hiyo kuwa awali ndge hiyo iltakiwa kutua kiwanjani hapo Novemba 7 lakini haikufika kutokana na sababu ambazo hazifahamu hadi hapo ilipotua Novemba 24 kiwanjani hapo bila kuwapo na tatizo lolote la kiusalama au kiufundi.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena Februari 26 mwaka huu(Leo) ambapo upande wa mashtaka utendelea kuleta mashahidi wake na washtakiwa ni pamoja na raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang'unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.
Mwisho.


Comments
Post a Comment