POLISI YANASA KIWANDA CHA KUTENGENEZA KONYAGI FEKI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitizama sehemu ya mbele ya kiwanda cha kutengenezea Konyagi feki ambapo muonekano wake ni maduka na saloon.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitembelea sehemu ya nyuma ya kiwanda cha kutengeneza Konyagi feki katika eneo la kambi ya raha Bomang'ombe wilayani Hai.
Sehemu ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda hicho zikiwa kituo cha polisi Bomang'ombe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha Pombe feki ya Konyagi  iliyokamatwa hivi karibuni wilayani Hai
Kamanda Boaz akiwa ameshikilia sehemu ya malighafi zinazotumika kutengezea Konyagi Feki.
Kamanda Boaz akionesha mihuri ambayo imekuwa ikitumika kuonesha tarehe ya kuanza na kumalizika kwa tarehe ya matumizi ya kinywaji hicho.
Kamanda Boaz akitizama Ndoo kubwa maarufu kama Diaba ambayo yamekuwa yakitumika kuchuja pombe hiyo kabla ya kuwekwa katika karatasi maalum.
Hivi ndivyo inavyoonekana pombe hiyo ikiwa na alama ya TRA.
Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa baada ya kukutwa wakifanya shughuli ya utengenezaji wa bidhaa hiyo feki.

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa kiwanda cha
kutengeneza Pombe "Feki" aina ya Konyagi huku likiwashikilia watu nane
waliokutwa ndani ya kiwanda hicho wakifanya shughuli ya utengenezaji
wa pombe hiyo.

Mbali na kiwanda na watuhumiwa hao pia Polisi imefanikiwa kunasa
mitambo mbalimbali iliyokuwa ikitumika kiwandani hapo zikiwemo
malighafi zilizokuwa zikitumika kufunga bidhaa hizo kabla ya kuuzwa
katika maduka ya jumla ya kuuzia Pombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishana mwandamizi msaidizi wa
polisi,Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Machi 14
mwaka huu majira ya saa 7:00 Mchana katika eneo la Kambi ya raha nje
kidogo ya mji wa Bomang'ombe.

 "Askari polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hawa baada ya
wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa utengezaji wa Pombe ambayo
haijaruhusiwa kisheria ikiwa na nembo ya Konyagi ndipo askari walianza
uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watu hao katika nyumba
inayomilikiwa na Elias Samson  mwenye umri wa miaka 31"alisema Boaz.

Kamanda Boaz alisema watuhummiwa hao pia walikutwa na lita 400 za
pombe ikiwa imehifadhiwa katika mapipa tayari kwa ajili ya kujazwa
katika vifungashio pamoja na Katoni 46 za pombe hiyo zote zikiwa na
nembo ya Konyagi.

Mbali na vitu hivyo Boaz pia alisema watu hao walikutwa na Makasha
tupu 178 ya kuhifadhi Konyagi yakiwa na nembo ,Pipa tupu 10
zinazoaminika kuhifadhia pombe hiyo wakati wa utengenezaji na Mihuri
miwili inayoonesha tarehe ya kutengezea na taraehe ya mwisho wa
matumizi ya bidhaa .

"Katika vitu vingine tulivyo wakuta navyo ni pamoja na majiko ya
mafuta "Ya Mchina"zaidi ya matano,vifaa vingine ambavyo ni kama Pasi
vilivyokuwa vikitumika kwa ajili ya kuchomea karatasi za nailoni baada
ya kujaza hiyo Pombe"alisema Boaz.

Kamanda Boaz aliyetembelea eneo kilipokuwepo kiwanda hicho aliwataja
waliokamatwa kuwa ni pamoja na George Kisivani (28), Yusuf George
(33), Preygod Urassa (27) na Richard Leonard (35) Hagai Nelson (38),
Jackson Shayo (29), Greyson Jonathan (27) wote wakazi wa Arusha pamoja
na Mohamed Rashidi (44) mkazi wa Dar es Salaam.

Makasha na vifungashio vyakutwa na alama ya TBS na TRA.

Katika hali isiyo ya kawaida Makasha ya bidhaa hiyo Feki yamekutwa
yakiwa na alama ya Ubora itolewayo na shirika la viwango Tanzania
,(TBS) huku karatasi zenye Pombe zikiwa zimebandikwa karatasi
inayotumiwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Kamanda Boaz alisema uwepo wa alama hizo mbili ni kutaka kumuaminisha
mnunuzi pamoja na mtumiaji wa bidhaa hiyo kuwa ni halali na
imethibitishwa na taasisi hizo mbili muhimu zinazosimamia Ubora wa
bidhaa pamoja na mapato.

Alisema uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini watengezaji wa
Makasha hayo,pamoja upatikanaji wa alama hizo za TRA huku akiongeza
kuwa mbali na kosa hilo la kutengeneza bidhaa bandia pia watu hao
wanashiriki katika kuhujumu Uchumi wa nchi.

 "Huu ni uhujumu Uchumi kwa sababu wametengeneza bidhaa feki ,harafu
wanaziuza madukani bila ya kulipia kodi,wakiwaaminisha wauzaji wengine
na watumiaji kuwa bidhaa yao imethibitishwa na TBS na wanalipa kodi
kwa kuweka alama ya TRA"alisema Boaz.

Kutokana na hali hiyo kamanda Boaz alisema tayari amefanya mawasliano
na Uongozi wa shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya
mapato nchni (TRA) ili kuondoa utata uliopo hku akiongeza haja ya
kutolewa kwa elimu ili kuzuia athari za matumizi ya bidhaa zisizokuwa
na ubora

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi


Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO