KINANA ,NYARANDU WAINGIA MKENGE.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama kwenye shamba la mkulima Khamis Idd (kushoto) katika Kijiji cha Mkenge, Jimbo la Singida Kaskazini, wakati wa ziara yake
ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akisaidia kuvuna mtama kwenye shamba la mkulima Khamis Idd katika Kijiji cha Mkenge, jimboni humo leo.
Kinana akiweka mtama kwenye mashine ya kupembua ambapo kwa saa moja hupata magunia 6 hadi 10 ya mtama.
Kinana akiwa katika vazi asili la viongozi wa kabila la Wanyaturu, akitoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Msange, wakati wa ziara yake Singida Kaskazini leo.
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu katika Kijiji cha Msisi. Singida Vijijini
Kinana na Nyarandu wakisaidia kuweka dirisha alipokagua ujenzi wa Kiwanda cha kukamua alizeti katika Kijiji cha Mtinko, Singida Kaskazini.
 Nyarandu akiteta jambo na Kinana wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mtinko


Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI AZINDUA MIRADI YA TANAPA CHAMWINO, DODOMA, AELEZA MIPANGO YA SERIKALI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA WANYAMAPORI WANAOVAMIA MAKAZI YA WATU