MAKOCHA WA FC BARCELONA WAWASILI KUTOA MAFUNZO KWA MAKOCHA WA TANZANIA.
CASTLE Lager, bia inayoongoza barani Afrika na FC Barcelona, moja kati ya timu kubwa
zaidi za soka duniani wameshirikiana kuleta makocha kutoka klabu hiyo
yenye makao yake huko Camp Nou, Hispania ili kutoa mafunzo ya mbinu
za soka kwa makocha wa Tanzania wiki hii. Makocha hao wa FC Barcelona
ambao wataendesha mafunzo hayo wamefika jijini Dar es salaam leo (31/8/2014).
Mafunzo hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam
kwa siku mbili zijazo ambazo ni tarehe 1 na tarehe 2 Agosti na yataendeshwa
na makocha waliobobea kwenye mbinu mbalimbali za kandanda ikiwemo Tiki
Taka. Makocha hawa ni Daniel Bigas Alsina and Isaac Oriol Guerrero Hernandez
kutoka Shule ya Soka ya FB Barcelona.
Mafunzo haya ni sehemu ya manufaa ya ushirikiano uliosainiwa mwaka
jana kati ya FC Barcelona na Castle Lager ambayo ni bia rasmi ya FC
Barcelona barani Afrika. Vilevile, mafunzo haya ni sehemu ya manufaa
ya ushirikiano huu kwa jamii.
Kupitia mafunzo haya, makocha 30 waliobahatika kutoka ligi kuu na
ligi daraja la kwanza watapata fursa maalum ya kujifunza mbinu mbalimbali
za mazoezi zinazotumiwa na FC Barcelona na kufanikiwa kuwatengeneza
baadhi ya wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi duniani.
“Tuna shauku kubwa sana kuona mafunzo haya yanakuja Tanzania na
tunafurahia kupata nafasi ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inatuunga
mkono. Tunaamini mafunzo haya yatawanufaisha makocha na wachezaji wa
Tanzania katika siku zijazo,” alisema Fimbo Buttallah, Meneja Masoko
wa Kampuni ya Bia Tanzania.
“Castle Lager ina historia kubwa na soka barani Afrika na tukio
hili litazidi kuimarisha uhusiano uliopo kati ya bia namba moja Afrika
na mchezo namba moja kwa kupendwa barani Afrika.”
Mafunzo haya kwa makocha yatahusisha mafunzo ya darasani kwa nadharia
na uwanjani kwa vitendo. Ikiwa ni sehemu ya mafunzo hayo, makocha
hao watatoa baadhi ya siri za mafanikio ya FC Barcelona ili kusaidia
kuleta utaalamu wa kimataifa kwenye soka la Tanzania.
Comments
Post a Comment