KUNDI LA WAMAREKANI WAJA NCHINI KUTIZAMA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji . Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji. Afisa Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi. Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Mount Meru, jijini Arusha kuh