MKWAJA FC MABINGWA WAPYA MWIDAU CUP 2014
Kombe la mshindi wa kwanza katika fainali ya kuwania kombe la Mwidau Cup 2014 iliyozikutanisha timu za Mkwaja Fc na Kimanga fc. |
Timu ya soka ya
Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga
timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliipigwa kwenye Uwanja
wa Mwera wilayani Pangani.
Mchezo huo ambao
ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga
ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za
awali toka mpira kuanza.
Mchezaji wa Mkwaja FC
Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake
mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko .
Hata hivyo
kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza
katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada
mlinda mlango wa Mkwaja.
Goli la pili la timu
hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa
timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk
80 Mkwaja FC kufunga bao la nne.
Akikabishi zawadi kwa
washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC
walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa, medali za
dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira.
Huku mshindi wa pili
ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba , seti
moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16
zikipatiwa jezi seti moja moja.
Awali akizungumza
kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji
vya soka katika wilaya hiyo
kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini.
Katika mchezo huo wa
fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said
Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.
Mwisho
Comments
Post a Comment