SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA
Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita. Safari ilianza kwa taratibu huku Mabalozi wakitizama mandhari tofauti ya uoto wa asili katika Mlima Kilimanjaro. Safari ya kuelekea Kileleni hivi ndivyo ilivyoendelea kuchukua kasi kwa Mabalozi . Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe akioneshwa moja ya kibao kilichokuwa kikielekeza muelekeo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro. Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe akipita katika moja ya daraja kuelekea eneo la Nusu njia. Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe alifika eneo la Nusu njia. Waziri wa mambo ya nje ya nchi,Mh Benard Membe akipata chakula na mkuu wa wilaya ya R