CCM YAWATIMUA CHENGE,TABAIJUKA,NGELEJA,CC YAWAKIMBIA TENA WAKINA LOWASSA,SOMA HAPA KUJUA
KAMATI kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM
/CC,imewazuia Viongozi wake waliochukua pesa kwenye Akaunt ya Escrow ya
kutoingia kwenye Vikao vya juu kwenye vya Chama hicho.
Viongozi waliozuiliwa ni Mbunge wa
Muleba kusini Profesa Anne Tibajuka,Mbunge wa Bariada Magharibi Adrew Chenge
pamoja Mbunge wa Sengerema William Ngeleja ambao wote kwa pamoja waliingiziwa
pesa na Mbia wa kampuni ya IPTL bwana james Rugimalira kupitia kwenye Akaunt ya
Benki ya Mkombozi.
Akitangaza Maazimio hayo ya Kamati ya
CC yaliyotakana na kikao kilichofanyika kwa siku moja Mkoani Dar Es Salaam,Mda
huu Hapa jijini Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi
CCM,Nape Nnauye wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema Kamati
ya cc imelijadili suala hilo kwamakini na kuwazuia viongozi hao wasiingie
kwenye vikao hivyo .
“Tumewataka viongozi hawa waliohusika
na mihamala ya Akaunt ya Escrow ambao ni viongozi,akiwemo mama Tibaijuka ambaye
naye ni mjumbe wa CC,Andrew Chenge mjumbe wa Nec na Ngereja pia ni wa Nec
wasiingia kwenye vikao hivyo mpaka pale suala hilo litakapotafutiwa
ufumbuzi”amesema Nape.
Nape Ameongeza kuwa suala lao
litajadiliwa na Kamati ndogo ya Maadili ya Chama hicho ambayo itachunguza na
kupeleka majibu haraka kwenye kamati kuu ya CC na kutolewa majibu.
Aidha,Kamati kuu hiyo ya CCM yaani CC
imewarushia mzigo Kamati ya Maadili ya chama hicho kuangalia adhabu ya Makada
wake waliotangaza nia mapema kama walikiuka adhabu waliyopewa ya kufungiwa kwa
miezi 12 kwa makada Sita wachama hicho walioanza kampeni mapema ya Urais ndani
ya chama hicho kabla ya mda kuanza.
“Kuhusu makada wetu waliotangaza nia
mapema ya kutanga uongozi mbalimbali hususani ya Urais tumeiachia Kamati ya
Maadili kuangalia kama walikiuka adhabu waliopewa au hawakukiuka,basi Kamati
hiyo inatakiwa itutoe majibu”amesema Nape.
Alibainisha kuwa Kamati hiyo ya
Maadili imeambiwa ianze kazi mara moja na ipeleke majibu kwenye kamati ya
Kuu.
Makada hao waliokuwa
chini ya adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri Mkuu mstaafu,
Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba, Waziri wa Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira na Mbunge wa Sengerema,
William Ngeleja.
Ambao inadaiwa Makada hao walipewa adhabu hiyo ya
onyo kali na Kamati Kuu Februari 18, mwaka jana baada ya kuthibitika kuanza
kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati kinyume na kanuni
za uongozi na maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
Vilevile baada ya kuhojiwa, walithibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.
Kutokana na adhabu
ya onyo kali makada hao kwa mwaka mzima walikuwa katika hali ya kuchunguzwa ili
kuwasaidia katika jitihada za kujirekebisha.
Vilevile Chama hicho kimepokea
masikitiko Mkubwa ya Msiba wa Mbunge wa Mbinga Mashariki Kaptain John Komba na
kusema ni pengo kubwa sana
Comments
Post a Comment