MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MH TEMBA NAYE AFIKISHWA KWA PILATO.
Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba
jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam
akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.
Kwa mujibu wa
Nipashe, Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya
hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.
Mheshimiwa Temba
alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu
chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe.
Aliwekwa chini ya
ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka
yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha
89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai.
Akisomewa mashitaka
na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka
huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion Iiliyopo Temeke jijini Dae es
salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu Godrey Deogratius ama Sulla.
Mshitakiwa alikana
mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana.
Hakimu Frank
alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March 11, mwaka huu,. Kabla ya
kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo cha polisi cha
Chang’ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu mlalamikaji kwa madai ya kuwa na
mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii huyo.
Ilidaiwa kuwa
mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na
sheria.


Comments
Post a Comment