Tizama:AZAM FC WAPOKELEWA NA GARI LA KUBEBA TAKA ZA KLABU YA EL MEREICK.
![]() |
| Hili ndilo basi ambalo El Merreikh wamewapatia Azam FC baada ya kuwasili Khartoum |
![]() |
| Basi aina ya Coaster ambalo wamepewa Azam FC Sudan |
WAWAKILISHI wa Tanzania
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamepata mapokezi ya
‘kigaidi’ mjini Khartoum , Sudan baada ya kuwasili usiku wa
kuamkia leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, El Merreikh.
Baada ya kuufuzu
mtihani huo, walikutana na visa zaidi walipotoka nje ya Uwanja wa Ndege,
kufokewa na watu waliokwenda kuwapokea, kabla ya kwenda kuwapakia katika basi
bovu na baya aina ya Coaster. Pamoja na hayo, Azam FC kwa kuwa walijua
watakutana na hali kama hiyo, hawakuonekana
kustaajabu, badala yake kuvumilia yote.
Mtendaji Mkuu wa
Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Khartoum kwamba
wamefanyiwa mambo ambayo kwa ujumla si ya kuanamichezo.
“Tunarekodi kila
kitu na tutatuma CAF (Shirikisho la Soka Afrika). Sisi hatuna wasiwasi nao, kwa
sababu tunawajua,”amesema.
Kikosi cha
wachezaji 23 wa Azam kimewasili Khartoum
tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni
mwa wiki.
Azam FC inahitaji
hata sare au kutofungwa kwa wastani wa zaidi ya bao 1-0 ili kusoga mbele kwenye
michuano hiyo, baada ya awali kushinda 2-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wiki
iliyopita.



Comments
Post a Comment