SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU KIJIJINI KISANGA.
Mgeni Rasmi katika Sherehe za uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akiongea na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica
Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na
kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo
Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa
Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia
kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi
na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua
Mama kiuchumi.
Mh. Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015
Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia
kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na
kumkwamua kiuchumi.
Akizungumza katika Sherehe hizo Mh.
Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia
wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi
kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe
sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa
kwanza atokee katika wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa
mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na
kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa
mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za
kisasa za kilimo bora.
Nae Mwakilishi kutoka Oxfam
Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa
wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi
mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha
Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni
Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa
vifaa na zana za Kilimo.
Eluka alizungumzia historia fupi
ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza
kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao
wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na
kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za
kuendesha Kilimo.
Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh.
Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na
watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano
hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano
la Mama Shujaa wa Chakula.
Comments
Post a Comment