ACACIA YAKUSANYA SHILINGI MILIONI 800 ZA KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU, BAADA YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (Katikati), akinyanyua juu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 800, baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampouni ya Acacia, Brad Gordon, (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye lango la kushukia kutyoka kilele cha Mlima Kilimanjaro, Mweka, Juni 28, 2015, Fedha hizo ambazo ni kwa ajili yab kusaidia sekta ya eli kwa watoto kutoka familia duni, zimetokana na wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kuchangisha fedha chini ya mpango wa kampuni hiyo wa "CanEducate". Kampuni ya Uchimbaji Acacia, inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, , imekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kupitia upandaji wa hisani wa mlima Kilimanjaro ambao unalenga kuchangisha fedha za kusaidia sekta ya elimu nchini chini ya mpango wa “CanEducate”, uliobuniwa na kampuni hiyo miaka mitano iliyopita. Timu ya wafanyakazi, marafiki na wanafamilia