HELKOPTA YA NYALANDU YANOGESHA KAMPENI ZA MGOMBEA MWENZA CCM

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la  Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la
Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi.Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCM Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCMHelkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua. Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua.Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta.Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua na helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua na helkopta.Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri. Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri.Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi.Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku. Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku.Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba. Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba.[/caption] Na Joachim Mushi, Singida MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea ya kuinadi ilani ya CCM. Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za wanaCCM na wananchi katika mkutano huo. Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia helkopta hiyo kwenye mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba Magharibi. Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura CCM kwani ndani ya ilani yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa maendeleo ya mkoa huo. Alisema endapo watachanguliwa watajenga kiwanda kikubwa cha kusafishia mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza thamani ya mazao kwa wakulima wa eneo hilo. Aliongeza kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia kitatoa nafasi za ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600 watapata ajira ndani ya kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya awamu ya nne kujenga shule za Sekondari za kata za kutosha na maabara ilani mpya ya CCM imepanga kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo ili ziweze kutumika kwa ufasaha. Bi. Suluhu alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya rufaa ambayo itakuwa ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani, pamoja na ujenzi wa barabara ya Ndago. Aidha akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi kufanya jitihada za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili kusongeza huduma kubwa za afya kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme vijiji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya pili. Aliongeza kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio la ukame aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo hayo. "...Serikali imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba ya kutosha, hivyo niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa njaa. Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza jimboni hapo alisema ilani ya CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji katika Vijiji vya Mgundu, Kinampanda, Makunda pamoja na vijiji vingine vinavyokabiliwa na kero ya maji. Alisema baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata kufanikiwa serikali itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa mabweni ili kuwanusuru watoto wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni pamoja huku wasichana wakikabiliwa na changamoto za kubebeshwa mimba na kukatishwa masomo yao. Mwingulu aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja za msingi na vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha. Bi. Suluhu anaendelea na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma akiinadi ilani ya CCM.

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/