MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI JIJINI DAR ES SALAAM



 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea.

Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
 Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 

"Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.


 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania, jijini Dar es Salaam. 
  
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam, 25 Febuari 2016: Kampuni ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora. . Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.
Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.

Maisha ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao.
“Dar es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.
Alisema Mh Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa vifaa vya Huawei.
Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia  yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa  kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29 mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki, spika za Bluetooth na tisheti.

Huawei Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.
Maduka yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.
Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana.
Maduka ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa  teknolojia  katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa
Kuhusu Huawei
Huawei ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500. Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.
Kampuni ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.
Huawei imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Kupata habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com
Hotuba ya Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Peter Philip
Uongozi wa Huawei
Wadau mbalimbali wa Huawei
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Nina furaha kubwa kuwa miongoni mwenu leo pamoja na timu nzima ya Huawei. Katika dunia ambayo teknolojia ya mawasiliano inabadilika kwa kasi kushiriki  katika mabadiliko hayo ya maendeleo ni upendeleo mkubwa.

Mabibi na Mabwana, Christine Qiang mwana Uchumi wa Benki ya Dunia alisema” Wigo wa simu za mkononi unakuwa kwa kasi, ukiwa ni njia moja kuu ya kutanua fursa za kiuchumi na huduma za msingi kwa mamilioni ya watu” Kuunganishwa kupitia Intaneti au simu za mkononi kunaleta taarifa za masoko, huduma za kifedha na huduma za kiafya sehemu za mbali zisizofikika kiurahisi na ina saidia kubadilisha maisha ya watu kwa namna za kipekee.

Mabibi na Mabwana Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza Huawei Tanzania kwa hatua hii nzuri katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania.

Sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania inakua kwa kasi na kuwa moja ya nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maendeleo haya ya kasi katika mawasiliano na teknolojia yamepelekea wawekezaji Wengi kuwekeza katika sekta hii nchini kwetu. Kwa sasa sekta hii inakua kwa kasi ya asilimia kumi na tano na asilimia ishirini kwa mwaka, kiwango ambacho kinaonyesha kua cha juu katika ukanda wa afrika mashariki.

Nchi Zaidi ya thelathini duniani hutengeneza simu za mkononi, hata hivyo ubora umekua alama ya utofautishaji katika makampuni haya ya simu. Kampuni ya Huawei imethibitisha mara kwa mara uwezo wao katika kuridhisha wateja wao kwa kuwapatia bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia ivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa.

Mabibi na Mabwana

Duka hili jipya na huduma matengenezo ya simu za mkononi la Huawei haliashirii ongezeko katika utajiri au mauzo yao ila inaashiria kutambua mahitaji ya wateja wao na fursa ya kupata bidhaa zenye uhakika na zilizo bora.

Nina Imani kuwa Huawei itaendelea kuwatosheleza wateja wake. Nchi ya Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi katika sekta ya teknolojia ivyo natumai na naamini Huawei watatumia fursa hiyo kuongoza soko la simu za mkononi nchini Tanzania.

Mabibi na Mabwana, Kwa mara nyingine nishukuru sana Uongozi mzima na menejimenti ya Huawei kwa kunishirikisha katika tukio hili tunapo fungua rasmi duka la Huawei na huduma za simu hapa J Mall.

Nina uhakika kila mteja atakae pita katika malango haya ya Huawei atapata kumbukumbu njema na mguso wa teknolojia ya uhakika.

Asanteni sana.

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/