TPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALITPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALI
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa
Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni
75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa
hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,.
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa
Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla
ya silingi milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha
wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza
hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa
Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100
Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na
Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano
hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba
Moshingi akiongea na wana-saccos wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kabla ya
kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/=kama mkopo ili kuinua mitaji yao.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa
Machibya.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta
Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni
Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule.
Comments
Post a Comment