WAFANYABIASHARA WA UTALII WANATANGAZIWA KUSAJILI NA KULIPIA ADA YA LESENI YA MWAKA 2016
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI
NA UTALII
WAFANYABIASHARA WA UTALII KUSAJILI NA KULIPIA ADA YA
LESENI YA MWAKA 2016
Wizara ya Maliasili na Utalii inawakumbusha wafanya
biashara za utalii wasiokuwa na leseni ya biashara hiyo inayotolewa kwa mujibu
wa sheria ya Utalii Na. 29 ya Mwaka 2008 Vifungu Na.10 na 31, kuwa wanatakiwa
kusajili na kulipia ada ya leseni kwa mwaka 2016 ifikapo tarehe 31 Oktoba,
2016.
Biashara za Utalii
husika ni hizi zifuatazo:
1
|
Kampuni za
kusafirisha watalii
|
10
|
Vivutio vya
kuuza bidhaa za urithi (Cultural heritage centres)
|
2
|
Kampuni za
uwindaji wa kitalii
|
11
|
Wajasiriamali wa
utalii wa utamaduni (Cultural tourism enterprises)
|
3
|
Wawindaji Bingwa
|
12
|
Kampuni za
kukodisha vifaa vya utalii
|
4
|
Kampuni za kusafirisha
watalii kwa ndege
|
13
|
Maeneo ya
michezo ya burdani (Theme parks, wildlife forms. Zoo, snake parks etc)
|
5
|
Kampuni za
kusafirisha watalii kwa Maputo (hot air balloon)
|
14
|
Kampuni za
kukodisha magari kwa watalii
|
6
|
Kampuni za
kusafirisha watalii kwa farasi
|
15
|
Kampuni za
kukatisha tiketi za ndege
|
7
|
Kampuni za kusafirisha
watalii kwa boti
|
16
|
Wakala wa kutoa
huduma kwa watalii (tourist handling agents)
|
8
|
Kampuni za
kupandisha watalii Milimani
|
17
|
Nyumba za huduma
za malazi (hoteli, loji, kambi za kitalii)
|
9
|
Kampuni za
utalii wa michezo ya kusisimua (tourism adventure sports)
|
18
|
Maduka ya zawadi
za kitalii (Curio Chops)
|
i.
Wizara
inachukua nafasi hii pia kusisitiza kwamba ni kosa linalostahili adhabu
kisheria kufanya biashara ya utalii bila ya kusajili na kulipia ada ya leseni
kwa mwaka husika.
ii.
Vilevile,
tunapenda kuwafahamisha kuwa maombi kwa ajili ya leseni ya kufanya biashara ya
utalii kwa mwaka 2017 yameanza kupokelewa katika Ofisi zetu zilizopo Dare s
Salaam, Arusha, Mwanza na Iringa.
iii.
Orodha
ya wafanyabiashara ya utalii waliosajiliwa na kulipia ada za leseni inapatikana
katika tovuti ya Wizara (www.mnrt.go.tz), na katika ofisi za Wizara zilizotajwa hapo juu.
Angalizo: Umma unatahadharishwa kutofanya biashara na kampuni za
biashara za utalii ambazo hazina Leseni ya Biashara ya Utalii ya mwaka 2016,
kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Simu: +255 22 2864230
Barua pepe:
ps@mnrt.go.tz
Comments
Post a Comment