MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI KANDA YA KASKAZINI.
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini ulitanguliwa na maandamano yaliyopita katika barabara mbalimbali za mji wa Moshi na kuhitimishwa katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Washiriki kutoka Asasi mbalimbali wakipita mbele na mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.
Baadhi ya viongozi wa taasisi mablimbali wakiwa wameketi meza kuu na mgeni rasmi wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini Said Mecky Sadiki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,Elizabeth Mushi akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatli wa kijinsia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Elizabeth Mushi akipeana mkono na Mgeni rasmi katika unzinduzi huo,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki mara baada ya kutoa taarifa juu ya ukatili.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki kutoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupina ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,uzinduzi iliofanyika katika viwanja wa vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi katika Shule ya Polisi Theresia Nyangasa akisoma taarifa juu ya vitendo vya kuutali na njia zilizoanza kuchukuliwa katika kukabiliana navyo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakifuatilia taarifa juu ya ukatili wa kijinsia iliyokuwa ikitolewa na viongozi wa Asasi mbalimbali .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa cheti kwa Kaimu Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita cha kutambua mchango wa jeshi la Polisi katika kupamban vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipena mkono kabla ya kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF Network) Grace Lyimo ,kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipeana mkono na Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wilaya ya Moshi,Elina Maro kabla ya kumkabidhi cheti kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya washiriki alipopita kugagua mabanda ya maonesho ya shughuli zinazofanywa na taaisisi zinazopambana na ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa TAWREF ,Dafrosa Itemba akitoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Moshi vijijini ,Hussein Jamal akizungumza wakati wa kikao cha makatibu kata na makatibu wa matawi kilichofanyika katika hotel ya King Size Himo. Mwenyekiti wa Makatibu katika jimbo la Vunjo ,Shaban Mwangi akisoma taarifa ambayo inadaiwa kupikwa kwa lengo la kukivuruga chama hicho katika jimbo la Vunjo. Baadhi ya viongozi wakisilikiliza kwa makini. Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa kikao hicho kilichokuwa na lengo la kurudisha hali ya amani na umoja ndani ya chama cha mapinduzi jimbo la Vunjo. Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilijadili pia tuhuma zilizotolewa dhidi yake. Makatibu wakila kiapo . Baadhi ya makatibu katika kikao hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji hicho. Mradi huo wa zahanati umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA Tsh. Milioni 25, Mbunge wa Jimbo la Mtera (Livingstone Lusinde) Tsh. Milioni 14.3 na Wananchi wa kjiji hicho Tsh. Milioni 12. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizindua mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lingstone Lusinde. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia) Hati ya Makabidhiano ya mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondar...
Comments
Post a Comment