EWURA YARIDHIA KWA SEHEMU OMBI LA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME
MAMLAKA
ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei
ya umeme kwa asilimia 8.5%.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni
kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha
maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari
mwaka 2017.
Akitangaza
bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema,
baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza
asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa
gharama za uzalishaji wake.
Shirika
la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar
limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.
Hata
hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao
hayazidi uniti 75 kwa mwezi.
Kundi la
TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na
tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.
Shirika
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme
na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme
nchini.
Comments
Post a Comment