DC SAME AAGIZA WANAFUNZI KUWA NA MITI YA KUITUNZA
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule
Na Mathias Canal
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule amewaagiza walimu wakuu
Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kusimamia zoezi la upandaji miti kwa
kumkabidhi kila mwanafunzi mti mmoja ambao atautunza katika kipindi
chake cha masomo.
Dc Senyamule
ametasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilayani humo
kilichohudhuriwa na walimu wote wa shule za msingi na sekondari,
Waratibu elimu, Maafisa Tarafa, Wazazi, Wanafunzi wawakilishi pamoja na
baadhi ya Viongozi wa dini.
Kikao hicho kilichokuwa na lengo la kukubaliana na
kupata namna bora ya kuboresha elimu na kiwango cha ufaulu Wilayani Same, Mkuu
huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo kwa namna maalumu kwa ajili ya wanafunzi
kufundishwa kwani mafanikio ya jitihada zao pekee katika kujisomea na
kufundishwa darasani haitoshi bali wanahitaji kuongezewa msukumo na utaalamu
zaidi kwa masomo ya ziada.
“Sote hapa kwa umoja wetu ni lazima tutambue kuwa
matokeo bora ya wanafunzi waliopo darasa la saba, wanafunzi wa kidato cha nne
na cha sita yapo mikononi mwa walimu hivyo njia bora ni kutatua matatizo yanayowakabili
walimu ili tuweze kufikia lengo” Alisisitiza Mhe Senyamule
Ameeleza kuwa endapo Changamoto za
makundi yote zitatekelezwa kwa kufuata utaratibu ikiwemo kila mmoja
kutumia nafasi yake ipasavyo katika kufuatilia mwenendo wa wanafunzi kwa
kuanzia Walimu, Serikali, Wazazi, na Wanafunzi Wilaya hiyo itakuwa na
matokeo makubwa katika matokeo yajayo.
Staki alisema kuwa Wilaya
ya Same imeanza imeanza kukua kielimu kupitia matokeo ya kidato cha pili
na cha nne kwani Wilaya hiyo imeshika nafasi ya 62 kati ya Halmashauri
184 ambapo kwa Mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 103.
Aidha katika
matokeo ya kidato cha pili Wilaya ya Same imeshika nafasi ya 37 kati ya
184 kwani mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 47.
Pia amewataka viongozi wote katika
kada mbalimbali kutumia vyema uongozi wao kwa kuwatumikia wananchi huku
akiwasihi kutumia lugha nzuri pindi wanapozungumza nao kwani kiongozi yeyote
atakayetumia lugha mbaya anapaswa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Sambamba na hayo
pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Same amepinga vikali matumizi ya Dawa za
kulevya ambapo amesema kuwa kwa Wilaya hiyo baadhi ya wananchi wake ni
wazalishaji wakubwa wa zao aina ya Mirungi ambalo pia limepelekea vijana
wengi kutumia huku wakijiweka kando na elimu kwa kuamini kulima zao
hilo sehemu ya mafanikio yao ya haraka.
Dc Staki amesema uongozi
wa Wilaya hiyo unaendelea na oparesheni ya kuteketeza matumizi ya
mirungi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na
matumizi ama uuzaji wa zao hilo.
Comments
Post a Comment