Posts

Showing posts from November, 2017

MTANDAO WA UTEPE MWEUPE (WHITE RIBBON) WAZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAORE JUUU YA VIFO VTOKANAVYO NA UZAZI KWA KINAMAMA NA WATOTO WACHANGA.

Image
Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maore wilayani Same wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon)   kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga . Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu  vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga . Mganga Mkuu wa wilaya ya Same,Dkt Godfrey Andrew akizungumza wakati wa mkutano na wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon) kujadili   vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga . Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu  vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga . Mkutano ukiendelea katika jengo la Mahakama lililopo katika kijiji cha Maore wilayani Same. Baadhi ya kina mama wakiwa na watoto w

MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya  ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na  Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.   Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)   Mkutano ukiendelea.     Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.  Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.   Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.   Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa w

SERIKALI YASISITIZA DESEMBA 31 KUWA UKOMO WA UWEKAGI WA VIGINGI (BEACONS) VYA MPAKA HIFADHINI

Image

SERIKALI YASISITIZA DESEMBA 31 KUWA UKOMO WA UWEKAGI WA VIGINGI (BEACONS) VYA MPAKA HIFADHINI

Image
Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili .......................................................................... Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesisitiza agizo la Serikali lililotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu kuhusu kukamilisha zoezi la uwekagi wa vigingi vya mpaka kwenye maeneo ya hifadhi nchini ifikapo Desemba 31 mwaka huu. Amesema lengo la kukamilisha zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini. Mhe. Hasunga ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi ya msitu wa Isalalo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo aliziagiza taasisi zilizo chini ya Wizara yake kukamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe hiyo ili kuiwezesha Serikali kubaini maeneo yenye mapungufu na kuyatolea uamuzi. “Ifikapo tarehe 31 tuwe tumemaliza kuweka hizo beacon (vigingi) za mipaka, baada ya hapo hatua itakayofuata, Serikali tu

HATUTAKUWA KIKWAZO CHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI - NAIBU WAZIRI JUMA AWESO

Image
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake haitakuwa kikwazo cha utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli ya kuwapatia wananchi majisafi na salama, bali itasimimamia utekelezaji wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija. Aweso alizungumza hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa Ruvuma, ambapo anakagua utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote mkoani humo. ‘‘Niwahakikishieni  wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, zaidi ya kuhakikisha miradi yote tunayoitekeleza inaleta tija na kumaliza kero ya maji kwa wananchi kulingana na maagizo ya Rais. Hivyo, lazima fedha zifike kwa wakati na zitumike kwa usahihi ili miradi yote ikamilike kwa wakati kulingana na mikataba,’’ alisema Naibu Waziri. ‘‘Ni jukumu langu kusimamia hilo na ninawaagiza watendaji wote wasimamie miradi yote hatua kwa hatua na watoe taarifa sahihi za maendeleo yake, ili sisi viongozi tujue changamoto

MADIWANI WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI

Image
Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Weruweru Swalehe Msenges.kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu. Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Mnadani  Nassib Mdeme ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu. Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akikabidhi cheti cha utambuzi kwa Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni wa kata ya Machame Magharibi ,Martin Munisi .kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha katika Hamlamahauri  hiyo ,Juma Massatu. Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbola Hai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilay

ANAYETAJWA KUWA MMILIKI WA SHULE YA SEKONDARI YA SCOLASTICA YA MKOANI KILIMANJARO AFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUSOMEWA SHITAKA LA MAUAJI.

Image
Mahakamani ya Hakimu mkazi ,Moshi. Anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya sekondari ya Scolastica,Edward Shayo akifikishwa katika mahakamani ya Hakimu mkazi ,Moshi. Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo akijiandaa kuingia chumba cha mahakama Jana. Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji ndogo wa Himo ,Edward Shayo na wenzake wawili ,Hamid Chacha ,Laban Nabiswa wakisindikizwa kuingia chumba cha mahakamani. Anayetajwa kuwa mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ,Edward Shayo na wenzake wawili wakitoka nje ya chumba cha mahakamani Mara baada yabkusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia . Mmoja wa ndugu wa kijana Humphrey Shayo akikia kwa uchungu wakati akitoka katika chumba cha mahakama Ndugu wa anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo wakionekana kwenye huzuni Mara baada kusomewa kwa mashtaka ya mauaji kwa ndugu yao hiyo Anaandika Dixon Busagaga wa globu y

STANDARD CHARTERED BANK MWENYEJI WA ‘ONE BELT- ONE ROAD’ (OBOR) AFRICA-CHINA ROADSHOW

Image
    Mgeni Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akihutubia waalikwa mbalimbali kuhusu fursa zinazopatikana katika uwekezaji. (OBOR Initiative) katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Stanchart bank jana,      Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya chakula cha jioni ambayo Standard Chartered Bank iliwaandalia wateja wake ambao ni wenyeji kutoka China.     Bw. Sun Chengfeng, Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania akizungumza na waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam     Mgeni rasmi Mh. Charles Mwijage Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji akibadilishana mawazo na Bw, Chengfeng , Mkuu wa kitengo cha uchumi na biashara ambaye ni mwakilishi wa China nchini Tanzania katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na standard charterd bank   Wawakilishi kutoka standard chartered bank c