SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU MKOANI SIMIYU .




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
Shirika la Hifadhi za Taifa leo limekabidhi mchango wa
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule tatu za vipaji
maalumu katika mkoa wa Simiyu za Simiyu Ufundi , Simiyu Wavulana na Simiyu Wasichana
.
Mchango huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.
Fedha hizi zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa shule maalum ya
sekondari ya ufundi mkoani Simiyu ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya mkoa katika
kuimarisha sekta ya elimu ambapo pia mkoa umepanga kuje nga shule nyingine
maalum mbili za sekondari za wasichana na
wavulana.
Kwa pamoja Mhe Mtaka
aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga waliahidi kuzitumia
fedha hizo kama zilivyokusudiwa na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika
kuhamasisha umuhimu wa wananchi kuheshimu sekta ya uhifadhi kwa kuwa ina manufaa
makubwa kwao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
aliahidi kuendelea kuwaunga mkono wana Simiyu kwa kuwa mkoa huo umekuwa mstari
sa mbele katika kusimamia sheria za hifadhi hususan Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kwa kuzuia uingizaji wa mifugo pamoja na majangili.
Shule ya Ufundi ya Simiyu inatarajiwa kugharimu kiasi cha
Shilingi Milioni 350 hadi itakapokamilika na wadau mbalimbali wameombwa kuunga
mkono jitihada hizo za Simiyu.
Mwisho .
Comments
Post a Comment