WABUNGE WA MIKOA YA KUSINI WAIMWAGIA SIFA SERIKALI NA TANESCO KWA KUMALIZA KERO YA UMEME MTWARA NA LINDI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu
kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, (wane kushoto),
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi, na
Mkuriugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, wakati alipowasili
kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi asilia (Mtwara Gas
Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018. Kituo hizo sasa
kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akitoka eneo la mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme wa Megawati 4 kila mmoja baada ya kuizindua, kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi Mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Wabunge wa Mikoa ya Kusini, wakiwa na mwenyekiti wao, Mhe. Selemani Bungara(wapili kushoto) |
NA MWANDISHI WETU, MTWARA-MEI 22,
2018
WABUNGE wa
bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara,
wameimwagia sifa Serikali hususan Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme TANESCO
kufuatia kumaliza adha ya umeme iliyodumu kwa takriban miaka 10 kwenye mikoa
hiyo.
Pongezi
hizo wamezitoa mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa, baada ya kuzindua Kituo cha Kuzalisha umeme wa gesi asilia (Mtwara
Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018.
Wa kwanza
kutoa pongezi hizo alikuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia chama cha Wananchi
CUF, Mhe
Maftah Nachuma ambaye yeye alienda mbali zaidi na kufikia kusema
atamuandalia Mhe. Waziri Mkuu mkutano mkubwa wa hadhara ili kuwaeleza wananchi
wa jimbo lake, mafanikio yaliyoletwa na serikali.
“Mheshimiwa
Waziri Mkuu, leo ninayofuraha kubwa sana, kwani kilio cha muda mrefu cha wana
Mtwara, cha kukosa umeme wa uhakika, hatimaye kimepatiwa ufumbuzi na kwetu sisi
hii ni sherehe kubwa, ningetamani mkutano huu ungewaalika na viongozi wengine
wa vyama vya siasa, na mimi binafsi nitakuandalia mkutano mkubwa wa hadhara ili
uje uwaeleze wananchi maendeleo haya yaliyoletwa na serikali.” Alisema Mhe.
Nachuma.
Naye
Mwenyekiti wa wabunge kutoka Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la
Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, alisema maendeleo haya ambayo serikali
inawafikishia wananchi ni kwa sababu bunge linaisimamia vema serikali.
“Siku zote
tunasema Kusini kwanza mambo mengine baadaye, na mimi niwaambie, tutaendelea
kupiga kelele hadi kero zote zitatuliwe, na niishukuru serikali kwa kumaliza
hii kero ya umeme iliyudumu kwa muda mrefu.” Alisema Mhe. Bungara
Naye
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia, yeye pia aliipongeza serikali kwa
kumaliza kero ya umeme Mkoani Mtwara, kwani sasa Mkoa wa Mtwara umekamilika kwa
kila eneo katika Nyanja ya uwekezaji.
“Mikoa
yetu ya Kusini tuna kila kitu, Gesi iko hapa, Bandari tunayo, Ardhi ambayo wala
haihitaji fidia nayo ipo, na sasa tunao umeme wa uhakika unaopatikana masaa 24,
hii ni fursa nzuri kwetu sisi tunaotoka mikoa ya Kusini.” Alisema Mhe. Hawa
Ghasia.
Akitoa
taarifa fupi ya kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema. Kituo cha kufua umeme kwa Gesi Asilia cha
Mtwara kilianza rasmi kufanya kazi mwaka 2007, kwa sasa kituo hiki kinazaidi ya
miaka kumi(10) na kina
uwezo wa kuzalisha Megawati 18 za umeme na ndio chanzo pekee cha Nishati ya umeme kwa
eneo lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara, isipokuwa kwa baadhi ya maeneo ya Wilaya
ya Kilwa na Liwale ambayo yanapata umeme kutoka kwenye vituo vyao vidogo.
“Mahitaji ya juu ya Nishati ya Umeme kwa eneo
lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara ni takribani Megawati 16.5”
Alisema Dkt. Mwinuka.
Alisema, Katika kukabiliana na changamoto ya kukua kwa mahitaji ya umeme katika
mikoa ya Lindi na Mtwara, serikali kupitia TANESCO ilifanya maamuzi ya upanuzi
wa kituo hiki cha kuzalisha umeme ili kukiongezea uwezo wake. Hatua hii
inahusisha usimikaji wa Mitambo miwili ya kufua umeme kila mmoja ukiwa na uwezo
wa kuzalisha Megawati 2, na hivyo kufanya ongezeko la jumla la Megawati nne (4)
Hatua
hii itaongeza uwezo wa kituo kuwa ni Megawati ishirini na mbili (22) ambao
utatosheleza mahitaji ya sasa ya eneo hili na kuwa na ziada.
Akimkaribisha
Waziri Mkuu kuzungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani alisema, Hatua
hii ni ya awali katika mpango endelevu unaolenga katika kuimarisha upatikanaji
wa nishati ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kiasi
cha Megawati nyingine nne (4) zitafuatia katika kipindi cha mwaka wa fedha
2018/2019, pia upo mpango mkubwa wa ujenzi wa mtambo wa Megawati 300 kwa msaada
wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Japani JICA, unaotarajiwa kukamilia ifikapo
mwaka 2020.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, aliwapa changamoto wakazi
wa Mkoa wa Mtwara kutumia umeme huo kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwani
sasa umeme ni bora na wa uhakika.
“Nitoe
wito kwa vijana, sasa mnaweza kufanya shughuli za kunyoa(saloon), kuchomelea
vyuma, kuranda mbao, kuuza juice, na hata wengine kuchaji simu na kuweka miziki
kwenye simu kwa kutumia computer, mnayo fursa kubwa ya kufanya shughuli zenu
ndogo ndogo za kiuchumi kupitia umeme huu ambao sasa unawaka masaa 24.”
Alisema.
Waziri
Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, kwa kuchangamkia haraka
uwepo wa umeme wa kutosha kwa kuanza kuweka taa za barabarani na hivyo kuufanya
mji wa Mtwara kung’aa majira ya usiku.
Mbunge wa jimbo la
Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe.Maftah Nachuma, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake.
Waziri Mkuu akipitia hotuba yake kabla ya kuhutubia.
Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Gesi Mkoani Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji ya Kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (katikati), Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (kulia) na viongozi wengine wa Mkoa wa Mtwara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi
wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya
Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo
sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi
wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya
Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo
sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.
Waziri Mkuu, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi na viongozi wa juu wa Wizara ya Nishati na Shirika hilo, wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi cha Mtwara Mei 21, 2018.
Wananchi wakishangilia
Mama akiwa ma mwanaye huku akifurahi
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughulikia uzalishaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia) na Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba.
Dkt. Kalemani akimnong'oneza kitu Meneja wa Kanda ya Kusini wa TANESCO, Mhandisi Aziz Salum.
Wafanyakazi wa TANESCO Mtwara
Waziri Mkuu Majaliwa na viongozi wengine wakifurahia burudani ya kwaya
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, wakiwa wenye furaha wakati vikundi vya burudani vikitoa burudani
Picha ya pamoja
Comments
Post a Comment