KAMA KIONGOZI HUFANYI KAZI YA KUMSAIDIA RAIS SAMIA HALAFU UNAIBUKA NA KUSEMA ETI MAKONDA ANAHOJI KAMA NANI, NIWAAMBIE MIMI NDIO MSEMAJI WA CCM SITAFUMBIA MACHO - MAKONDA



SONGWE 

"Viongozi wote iwe ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu au Ofisi yoyote ile ndani ya Nchi yetu ya Tanzania yawapasa kufanya kazi kikamilifu, wapo baadhi ya Viongozi wao wanakaa tuu maofisini Dodoma au Dar es salaam na kula viyoyozi tu, fanyeni ziara mkague watendaji wote na muache tabia ya kukombatiana na kufichiana siri"

"Tembeeni na sio kusubiria CCM ikija kwenye mikutano hii mnaanza kufunga tai na kuanza kuongea ooh anaongelea sheria kama nani ? nawajibu kuwa Naongelea kama Mtanzania"

"CCM tunataka kila Mwananchi ahudumiwe na sio kutishana na mimi sitishiki kabisa mnatakuwa kukumbuka kwamba hata hiyo mishahara mnayopewa ni kodi ya Watanzania"

"Mimi ndio msemaji wa CCM na ninasema kwa niaba ya Mwenyekiti wetu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nimeapa nitasema ukweki bila kumung'unya maneno na kama mnadhani nitakufa sasa ..hapana Mungu wetu wa upendo bado ananihapa Afya njema"

"Wapo baadhi ya Viongozi wapo Serikalini wanakula vizuri, wana hela, magari ya kifahari na majumba makubwa ya kifahari halafu hata kazi ya kumsaidia Rais Dkt. Samia hawaifanyi na wengine mnasubiria Rais aje ndio mjitokeze na kumdanganya kuwa mama tunaupiga mwingi wakato anatoa fedha za miradi na hamfanyi kazi zaidi mnamchonganisha tu na Wanachi"

"Hufanyi kazi ya kumsaidia Rais Samia halafu unaibuka kusema mnashangaa eti Makonda anahoji...bado mtashangaa sana ni lazima mumsaidia kazi kama watumishi wa Serikali na sisi huku kwenye Chama hatutafumbia macho watumishi wazembe"


Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO