BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI


 BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI

#KAZIINAONGEA

 Katika kuendelea  kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.

  Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi.

Aidha Katika vitongoji 1849 vya  Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.


Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/