EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Equity For Tanzania Limited- EFTA Bwana Nicomed Bohay akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzindunzi wa Hati Fungani za EFTA tukio lilofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency. 
Wageni mbalimbali, wakiwemo wadau wa sekta ya fedha, wawekezaji na wawakilishi wa taasisi za kifedha, wakifuatilia kwa makini tukio la uzinduzi wa EFTA Corporate Bond ya Shilingi bilioni 50, lililofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliashiria hatua mpya ya kuimarisha upatikanaji wa mtaji wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji nchini.

Wajumbe wa jopo la majadiliano wakichangia mada wakati wa uzinduzi wa EFTA Corporate Bond ya Shilingi bilioni 50 jijini Dar es Salaam, wakijadili umuhimu wa mtaji wa muda mrefu katika kuimarisha sekta za uzalishaji na kukuza masoko ya mitaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA, Nicomed Bohay, akichangia mjadala wa jopo wakati wa uzinduzi wa Hati Fungani ya Sh bilioni 50 jijini Dar es Salaam, akieleza namna mpango huo unavyolenga kuimarisha mtaji wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji na kutoa fursa ya uwekezaji kwa umma.
Wageni mbalimbali, wakiwemo wadau wa sekta ya fedha, wawekezaji na wawakilishi wa taasisi za kifedha, wakifuatilia kwa makini tukio la uzinduzi wa EFTA Corporate Bond ya Shilingi bilioni 50, lililofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliashiria hatua mpya ya kuimarisha upatikanaji wa mtaji wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji nchini.
Muhumiza Buberwa, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya CRDB, akizungumza wakati wa uzinduzi wa EFTA Corporate Bond jijini Dar es Salaam, akieleza umuhimu wa ushirikiano kati ya benki na masoko ya mitaji katika kuimarisha ufadhili wa sekta za uzalishaji nchini.
Meneja wa Maendeleo ya Soko kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), David Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa EFTA Corporate Bond jijini Dar es Salaam, akisisitiza umuhimu wa masoko ya mitaji katika kuhamasisha mtaji wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji nchini.
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu na Sheria wa Equity for Tanzania Limited (EFTA), Lucy Bwana, akifuatilia kwa makini uzinduzi wa EFTA Corporate Bond ya Shilingi bilioni 50 uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam, tukio lililolenga kuimarisha upatikanaji wa mtaji wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji nchini.
Wafanyakazi wa Equity for Tanzania Limited (EFTA) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa EFTA Corporate Bond ya Shilingi bilioni 50 jijini Dar es Salaam, wakionesha mshikamano na dhamira ya kuimarisha ufadhili wa muda mrefu kwa sekta za uzalishaji nchini.

EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50

Na Dixon Busagaga, Dar es Salaam

Kampuni ya Equity for Tanzania Limited (EFTA) imezindua rasmi Hati Fungani ya Shilingi bilioni 50, hatua inayotajwa kuwa kichocheo cha kuunganisha masoko ya mitaji na sekta halisi za uzalishaji kama kilimo, usafirishaji na viwanda.

Uzinduzi huo umeofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, uliwakutanisha wadau wa sekta ya fedha, wawekezaji na taasisi mbalimbali za kifedha, huku ujumbe mkuu ukiwa ni kuimarisha upatikanaji wa mtaji wa muda mrefu kwa shughuli zinazozalisha mapato.

Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA, Nicomed Bohay, alisema Hati Fungani hiyo imelenga kuhakikisha kampuni inapata mtaji wa muda mrefu unaoendana na maisha ya mali zinazofadhiliwa.

“Tunafadhili mali kama matrekta, magari ya biashara na mitambo ya viwandani ambayo huzalisha mapato kwa miaka kadhaa. Kupitia Hati Fungani hii tunahakikisha tunapata mtaji wa muda mrefu unaoendana na maisha ya mali hizo,” alisema Bohay.

Kwa mujibu wa Bohay, fedha zitakazokusanywa zitaelekezwa moja kwa moja katika kupanua huduma za ukodishaji wa mali (leasing) kwa wakulima, wasafirishaji, wakandarasi pamoja na wafanyabiashara wadogo na wa kati. Lengo ni kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kuwapatia zana na mitambo inayowawezesha kufanya kazi kwa tija zaidi.

Mchumi wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Andrew Temu, alisema upatikanaji wa mtaji wa muda mrefu ni nyenzo muhimu katika kuchochea mapinduzi ya uzalishaji barani Afrika.

“Afrika haina tatizo la uhitaji wa vifaa vya uzalishaji; changamoto ni namna ya kuvipata. Taasisi kama hizi zikipewa mtaji wa muda mrefu, zinaweza kusaidia wakulima na wajasiriamali kupata mitambo kwa urahisi zaidi,” alisema Prof. Temu.

Aliongeza kuwa mitaji ya muda mfupi mara nyingi haiendani na mahitaji ya uwekezaji katika sekta za uzalishaji, hasa kilimo na viwanda, ambavyo vinahitaji muda mrefu ili kurejesha faida. Hivyo, uwepo wa Hati Fungani kama hii unasaidia kuleta uwiano kati ya muda wa uwekezaji na muda wa marejesho.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) David Magabe alisema utoaji wa Hati Fungani unaongeza kina cha soko la mitaji na kusaidia kuelekeza akiba za ndani kwenye shughuli za uzalishaji, badala ya kubaki katika mifumo ya uwekezaji isiyogusa moja kwa moja uchumi halisi.

Hati Fungani hiyo inatoa riba ya ushindani ya asilimia 14 kwa mwaka na uwekezaji unaanzia Shilingi 500,000, hatua inayolenga kupanua ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji unaochochea sekta za uzalishaji.

Kwa kuunganisha mitaji ya wawekezaji na mahitaji ya wakulima, wasafirishaji na wamiliki wa viwanda, uzinduzi wa Hati Fungani ya EFTA unaashiria hatua mpya ya kutumia masoko ya mitaji kama daraja la kuimarisha uchumi halisi wa Tanzania.

Mwisho


Comments

Popular posts from this blog

CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAZINDUA KITUO CHA KUTOA MSAADA WA KISHERIA

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.