MAALIM SEIF, PROFESA LIPUMBA WAPETA TENA UCHAGUZAI WA CUF, JUMA HAJI DUNI MAKAMU MWENYEKITI
Viongozi wakuu wa CUF wakionyesha mshikamano baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Wa pili kulia ni msimamizi wa uchaguzi huo Awadh Ali Said (Picha na Salmin Said, OMKR) Na Hassan Hamad (OMKR) Mkutano Mkuu wa CUF Taifa umemchagua tena Katibu Mkuu wa Chama hicho kuendelea na wadhifa huo kwa kupata kura 675, sawa na asilimia 99.5 ya kura zilizopigwa. Mkutano huo pia umemchagua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa kupata kura 659 sawa na asilimia 95.5 na kumshinda mpinzani wake Chifu Lutalosa Yemba aliyepata kura 30 sawa na asilimia 4 nukta 3. Aidha mkutano huo umemchagua Mhe. Juma Duni Haji kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kupata kura 662 sawa na asilimia 99.25. Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, amewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumpa tena ridhaa ya kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. ...