Posts

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIANA NA TANZANIA KUINUA ELIMU

Image
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma. Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu. Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia. Mradi huo umelenga kuon...

KADAMA MALUNDE ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA.

Image
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC) Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi mjini Shinyanga   Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia) Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang'anyi akizungumza baada ya uchaguzi, kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Ste...

CHADEMA MOSHI MJINI WAMPITISHA JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO

Image
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini. Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburoakizungumza wakati wa mkutano huo. Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini,Joel Makwaia akizungumza katika mkutano wa Chadema alipoalikwa kukiwakilisha chama chake. Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo. Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Moshi mjini,Leonard Buberwa akizungungumza akati wa mkutano wa kumpata mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini. Watia nia katika nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini,Basil Lema,(kushoto) Jafary Michael (katikati) na wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko  wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza. Mbunge wa iti ...

WATIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI KUPITIA CCM WAJINADI MBELE YA WAJUMBE KATA YA MAWENZI.

Image
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo akijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi. Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mawenzi wakiwasikiliza wagombea. Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Edmund Rutaraka akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi. Baadhi ya wajumbe katika kata ya Mawenzi. Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Patrick Boisafi akiomba kura mbele ya wajumbe wa kata ya Mawenzi, Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Chief Omary Mwaliko akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata a Mawenzi. Omary Mwaliko akipongezwa na wanachama a chama hicho mara baada ya kutoa maelezo yake katika mkutano huo uliofanyika katika uwanja wa Hindu Mandal. Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha aijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi. Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Msohi mjini,Athuman Ram...