Posts

TANGAZO LA MSIBA WA MAMA JUDITH TARIMO

Image
Familia ya Marehemu Cyprian Tarimo ya Ukonga, Mombasa Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Mama Judith Tarimo kilichotokea Oktoba 25,2015 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mombasa na Rombo Mahida, Mkoani Kilimanjaro.  Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki wote wa ukoo wa Tarimo na Shayo, popote pale wa lipo.  Mwili wa marehemu unataraji kuagwa Oktoba 28,2015 kabla ya kusafirishwa siku hiyohiyo kwenda Mahida Rombo kwa maziko Alhamisi Oktoba 29,2015. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA YESU LIHIMIDIWE AMEN.  

KIPINDI KIPYA CHA DANGA CHEE KURINDIMA CHANNEL 10 KILA ALHAMISI SAA NNE USIKU

Image

WALIOSAMBAZA MATOKEO YA URAIS KINYUME CHA SHERIA WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam leo. Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo. Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia. Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo.  Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo. Na Dotto Mwaibale WATU wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Ke...

MBATIA ,KOMU WATAKATA MOSHI VIJIJINI NA VUNJO

Image
 

POLISI KILIMANJARO WAPIGA ZOEZI KWA AJILI YA UCHAGUZI SIKU YA KESHO.

Image
Baadhi ya viongozi wa ngazi ya Juu Katika jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya mazoezi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro.Fulgence Ngonyani akipokea taarifa fupi toka kwa kiongozi wa kikosi cha kutuliza ghasia. Askari Polisi wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika zoezi maalum. RPC Ngonyani akiongoza matembezi ya askari Polisi ikiwa ni sehemu ya mazoezi. Kikosi cha kutuliza Ghasia ,FFU. Matembezi yakiendelea kupita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi. Asakari Polis wakiimba nyimbo katika zoezi hilo. Wakati mwingine mchakamchaka ulichukua nafasi. Hatimaye mazoezi hayo yakafikia tamati katika viwanja vya Polisi vilivyoko katika ofisi za FFU. Baadhi ya viongozi wa jeshi hilo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

TUPIGE KURA, TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI

Image
TUPIGE KURA, TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania inafanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, hii ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe. Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964. Uchaguzi wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi  waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao w...

JESHI LA POLISI MBEYA LAPIGA MARUFUKU KWENDA KUPIGA KURA UKIWA UMEVAA SARE ZA VYAMA

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limetoa rai kwa wafuasi wa vyama vishiriki katika uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu kujiepusha kufika katika kituo cha kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zenye picha za wagombea, maneno au nembo ama rangi za chama cha siasa. Aidha wametakiwa , kuepuka kutumia uvumi, maneno ya uongo, hisia au visingizio vyenye lengo la kuwazuia wengine kwenda kupiga kura. Pia amewataka  kuepuka kufanya kampeni katika kituo cha kupigia kura iwe kwa maneno ya ushawishi au kwa kuonyesha ishara ya chama fulani cha siasa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ahmed Msangi amesema nivema kila mwananchi anae stahili kupiga kura ahakikishe anafuata taratibu hizo ili kujiepusha na vitendo vya uvujifu wa amani katika siku hiyo muhimu. Amesema  vyema kila mwananchi kupiga kura kwa kutumia jina na kitambulisho chake na sio cha mtu mwingine, aliyekufa au mgonjwa, kuepuka kufany...