Posts

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MAULID DAR

Image
 Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Go for Zanzibar (GOZA) a German NGO supports the Welezo Old Age Home

Image
Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi  msaada Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar  Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax  na mwaka mpya  kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma na Hassan Khamis hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao welezo jana Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi  msaada Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar  Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax  na mwaka mpya  kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao welezo jana Mwakilishi wa Wazee Welezo Mzee Shein, akimshukuru Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleische, kw...

AKINA MAMA NA VIJANA NI NGUZO KUBWA YA KULETA MABADILIKO KATIKA VIJIJI.

Image
 Bwana Bony Lukas akieleza jinsi anavyofanya uraghbishi hasa katika kuwasaidia vijana kujua haki zao na kujitambua. Na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa Ni suala ambalo lipo wazi kuhusu tofauti za kimaisha baina ya wakazi wa mijini na vijijini, ila changamoto nyingi zaidi zinaonekana kuwakabili zaidi wale wanaoishi vijijini. Huko wananchi wanakosa huduma ambazo kimsingi ni haki zao na hivyo kutokuwa na usawa baina yao na wale wa mijini. Picha kubwa inayojionesha vijijini kwa upande wa wanawake ni hasi kwa kiasi Fulani ukilinganisha na ile ya wanaume. Usawa wa kijinsia na kielimu baina yao na wanaume ni mkubwa sana, kesi za unyanyasaji kwao ni nyingi zaidi.   Pamoja na jihudi nyingi za kuwawezesha wanawake bado hawajapata nafasi ya kutoshwa kuweza kusikilizwa. Wanaume wameendelea kuwa watoa maamuzi na wanufaikaji wa kimfumo.   Mmoja wa waraghbishi akiwa anaonesha ripoti ya wanafunzi watoro katika shule ya msingi ya Nyandekwa . Takwimu zinaonesha kuwa hata...

Raia Waamirifu wilayani Kahama Wakerwa na Utoro

Image
  Pichani nikiwa nazungumza na   Raia waamilifu kutoka kijiji cha Kilago  wilayani Kahama ambapo nilipata nafasi ya kujua mambo  mbalimbali ikwemo mchango wa uraghabishi  katika kijiji hicho katika sekta ya elimu  Na Krantz Mwantepele , Kahama Utoro ni tabia ya kuondoka au kutokufika mahali mara kwa mara bila ya kutoa taarifa. Tabia hii ipo kwenye maeneo ya makazini pamoja na shuleni. Katika baadhi ya kata za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Tabia hii imekuwa kero kwa wanajamii wa kata za Nyandekwa na Kilago kwa kuwa inawarudisha nyuma kimaendeleo. Wakiwa kama sehemu ya wananchi wa kata hizo, waraghbishi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto watoro wanahudhuria shuleni. Ikiwa kama sehemu ya uraghbishi, kutambua changamoto zinazokabili jamii wanayoishi, waraghbishi walitambua kwamba hili ni tatizo na hivyo kuamua kulishughulikia. “Nikiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zangu, nikakuta watoto wamejibanza kwenye kichaka, na wen...

UDHAIFU WA USIMAMIZI WA MIRADI MBALIMBALI NI CHANGAMOTO KATIKA KULETA KASI YA MAENDELEO NDANI YA JAMII

Image
Waraghbishi toka kijiji cha Pandagichiza wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya tanki la maji, ambalo baadhi yao ndio wasimamizi wake kutokana uaminifu wao. Tanzania ya leo, imepitia mabadiliko mengi yanayogusa kila sekta tangu ilipojikomboa na kuwa nchi huru baada miaka 53 ya utawala wa kikoloni. Kwa mfano, katika kipindi hicho hadi sasa, nchi imeshuhudia kuimarika kwa huduma mbalimbali za kijamii. Kwa uchache, huduma hizi ni pamoja na   afya, elimu, demokrasia, utalii, viwanda na miundombinu mbalimbali.   Katika sekta ya elimu, ongezeko kubwa la shule kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu limeshuhudiwa. Hii ni moja ya hatua kubwa kuwahi kufikiwa tangu nchi ilipoanza kujitawala. Katika sekta ya afya, hospitali, zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi kutegeme mahitaji ya watu. Miundombinu ya barabara imeimarika maradufu na kuifanya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kuwa na barabara zenye lami kwa kilomita nyingi. Lakini pamoja na mafanikio hayo, nch...

Waraghbishi wawawezesha wanakijiji kujua haki na wajibu wao

Image
Na Krantz Mwantepele. Tanzania ya leo, imepitia mabadiliko mengi yanayogusa kila sekta tangu ilipojikomboa na kuwa nchi huru baada miaka 53 ya utawala wa kikoloni. Kwa mfano, katika kipindi hicho hadi sasa, nchi imeshuhudia kuimarika kwa huduma mbalimbali za kijamii. Kwa uchache, huduma hizi ni pamoja na  afya, elimu, demokrasia, utalii, viwanda na miundombinu mbalimbali. Katika sekta ya elimu, ongezeko kubwa la shule kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu limeshuhudiwa. Hii ni moja ya hatua kubwa kuwahi kufikiwa tangu nchi ilipoanza kujitawala. Katika sekta ya afya, hospitali, zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi kutegeme mahitaji ya watu. Miundombinu ya barabara imeimarika maradufu na kuifanya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kuwa na barabara zenye lami kwa kilomita nyingi. Lakini pamoja na mafanikio hayo, nchi imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali katika kila hatua ya kujaribu kuboresha huduma na mahitaji ya kijamii. Miongoni mwa cha...