Posts

MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QURAAN TUKUFU KUFANYIKA DIAMOND JUBILEE JUMAPILI HII

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID MASHINDANO ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo, Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya kutekeleza ibadaya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifa mbalimbali...

RAIS KAGAME KUFUNGUA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM-2016

Image
Ofisa Mawasiliano Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu maonesho  ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho hayo. Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Mkutano na wanahabari ukiendelea. Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Na Dotto Mwaibale RAIS Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kuanza Juni 28,2016 hadi J...

HARAMBEE YA OKOA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIKA LEO MKOANI DODOMA

Image
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun. PICHA NA MICHUZI JR. Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waand...

MAOFISA 27 WA NGAZI ZA JUU KATIKA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) WAMALIZA MAFUNZO YA KIJESHI KATIKA KAMBI YA MLELE MKOANI KATAVI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akipokea salamu wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa maofisa 27 wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikagua gwaride la maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakati wa kufunga mafunzo yao katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. Maofisa wa ngazi za juu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) wakila kiapo cha utii wakati wa kumaliza mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika kambi ya Mlele mkoani Katavi. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa TANAPA,Witness Shoo wakifuatilia maonesho ya kijeshi kutoka kwa maofisa wa ngazi za juu wa shirika hilo waliomaliza mafunzo katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe na wageni wengine waalikwa wakiangalia umahiri wa ...