Posts

WAFANYAKAZI WA NMB TAWI LA NELSON MANDELA WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI MJINI MOSHI LEO.

Image
Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo. Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakivuka barabara tayari kuanza zoezi la kufanya usafi katika eneo la Double Road mjini Moshi leo. Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi katika maeneo ya maduka yaliyopo eneo la Double Road mjini Moshi. Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kishosha akiowaongoza wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi . Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakiokota taka zilizokusanywa wakati wa zoezi la usafi lilofanyika katika eneo la Double Road mjini Moshi. Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa na taka zilizokusanywa wakienda kuzitupa katika eneo la kusanyia takataka. Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiendelea na usafi kati...

Tigo yakabidhi madawati ndani ya msimu wa fiesta wilayani Kahama

Image
Mkurugenzi  wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa wilaya ya Kahama  Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta. Wanafunzi  wa shule ya Msingi Mungula wakiwa wamekaa kwenye madawati baada ya kuyapokea madawati 235 kutoka kwa Kampuni ya Tigo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga Mkurugenzi  wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (wa kwanza kulia ) akiwa amekaa kwenye madawati baada ya makabadhiano anayefuatia ni  Mkuu wa wilaya ya Kahama  Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta.

RC SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka, Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia)   akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata...