Posts

KATIZO LA UMEME - MKOA WA KINONDONI KUSINI MWISHO WA WIKI HII

Image
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:- TAREHE:     Jumamosi 01 Oktoba, 2016 MUDA:        02:00 Asubuhi hadi 11:00 jioni SABABU:    Kujenga laini mpya ya Mburahati na ukarabati wa laini za Tandale Textile ili                    kuboresha hali ya umeme. MAENEO YATAKAYOATHIRIKA: Maeneo yote ya Tandale, Manzese, Sinza Uwanja wa TP, Sinza Vatican, Namnani Hotel, Iteba, Sinza Kijiweni,   Sinza Kumekucha, Sinza Mwika, TTCL Manzese , Urafiki Quarters, Urafiki Textile,TSP Ltd Millenium business, Sinza Lion Hotel, Rombo Sunflower, Strabag compound, Engen petrol station, Masamaki Plastic Bags Ltd pamoja na maeneo ya jirani. TAREHE:      Jumapili 2 Octoba, 2016 MUDA:        0...

ZIMWI LA TEGETA ESCROW LAMTISHA PROFESA TIBAIJUKA, AKATAA KUPOKEA DOLA 300,000 BAADA YA KUPEWA TUZO YA KIMATAIFA

Image
  Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam .   Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.  Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.   wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Mkutano na wanahabari ukiendelea. Na Dotto Mwaibale MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN),  kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta. Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al Khalifa. Akizungumza jana ...

TAREHE YA MWISHO YA UFUNGAJI WA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI (EFPP) KWENYE VITUO VYA KUUZA MAFUTA NCHINI

Image
Kufuatia changamoto zilizojitokeza katika zoezi la ufungaji wa mashine za kielektroniki zinazojulikana kama Electronic Fuel Pump Printer (EFPP) kwenye Vituo vya kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa na kufuatia agizo la Serikali kuwa wamiliki wa vituo vyote wawe wamefunga mashine hizo ifikapo tarehe 30 Septemba 2016, Wizara ya Fedha na Mipango, Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Chama cha Wamiliki na  Waendeshaji wa Vituo vya Kuuza Mafuta Nchini (TAPSOA) umekutana na kujadiliana changamoto zilizopo katika zoezi la ufungaji wa mashine za EFPP na  kukubaliana yafuatayo;- a)Serikali imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kufunga mashine za EFPP, ili kutoa nafasi kwa TRA ikishirikiana na TAPSOA kutatua changamoto  zilizopo kwa sasa. b)Wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta ambao hawajakamilisha ufungaji wa mashine za EFPP waendelee kutumia mashine za mkono (ETR) mpaka hapo watakapotaarifiwa vinginevyo. c)TRA inawakumbusha wa...

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MBILI MPYA ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWA AJILI YA ATCL JIJINI DAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiingia kwenye ndege mojawapo baada ya kukata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja...