Posts

NAPE,MBOWE WAONGOZA KUUAGA MWILI WA MPOKI BUKUKU DAR

Image
 Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa akiwa ameshika shada la maua alipokuwa akiingiza kwenye gari lenye jeneza la mwili wa marehemu Mpoki Bukuku  Mpigapicha Mkuu wa Gazeti l...

SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI

Image
  Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki, ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Rais John Magufuli azidi kupunguza Baraza la Mawaziri kufikia 15 na Kamati Kuu 15 pamoja na Halmashauri Kuu wajumbe 55. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffar Sabodo, amemshauri Rais John Magufuli kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, akisema hali hiyo itamsaidia kuleta tija zaidi katika utendaji wake. Aidha, Sabodo amemshauri Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM. Akizungumza katika mahojiano maalumu na JAMBO LEO nyumbani kwake Dar es Salaam, Sabodo alisema hatua hiyo itasaidia Serikali kutekeleza falsafa yake ya kubana matumizi. “Kupungua kwa ukubwa wa Baraza la Mawaziri kutajenga uwajibi...

SAFARI YA MWISHO YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KATIKA KITUO CHA KIBO KABLA YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU

Image
Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza . Safari ilivyoendelea hali ya hewa ilibadirika arikadhalika uoto wa misitu mifupi ulianza kutoweka kadri safari ilivyoenedelea. Safari iliendelea kwa motto wa "Mdogo Mdogo". Wakati mwingine  kulihitajika maneno ya faraja ili kufanikisha safari hii. Eneo hili ndilo la mwisho katika Mlima Kilimanjaro kuona maji yakitiririka wakati wa safafri ya kupanda Mlima Kilimnjaro. Kutokana na kubadirika kwa hali ya hewa ,washiriki wengine walivalia vizuia upepo,wenyewe walivipa jina "Shilawadu". Baadae uoto wa misitu ukatoweka kabisa ,safari ikawa ni ya kupita katika eneo la jangwa likijulikana kama Saddle. Safari iliendelea ya kufika kituo cha mwisho cha Kibo Hut. Wenye kuhitaji Msaada ,walipata msaada. Mapumziko kwa ajili ya kupata Chakula yalifanyika katika eneo la Saddle. Safari iliende...

TAASISI YA UTAFITI YA MAGONJWA YA BINADAMU KILIMANJARO (KCRI) YAWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA UPENDO NA WALIOLAZWA KCMC

Image
Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi walizopeleka katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Upendo cha mjini Moshi. Zawadi ya Kei iliyotolewa kwa watoto wa kituo cha Upendo cha mjini Moshi. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro,(KCRI) Profesa Blandina Mbaga akisalimiana na Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi Sister Yasinta walipofika kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho. Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi,Sister Yasinta Diwi akiwaeleza historia ya kituo hicho wafanyakazi wa taasisi ya utafiti ya magonjwa ya binadamu Kilimanjaro (KCRI). Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina Mbaga akizungumza na Mkurugenzi wa fedha Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Hilda Mungure (katikati) na Elizabeth Msoka. Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Uta...