PSPF YATOA SEMINA KWA MAAFISA WA POLISI WANAWAKE KWENYE MKUTANO WA SHIRIKA LA MAJESHI YA POLISI KUSINI MWA AFRIKA SARPCO
Afisa mwandamzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kushoto), akitoa mada iliyoelezea faida mbalimbali amzipatazo mwanachama wa Mfuko huo kwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya maafisa polisi wanawake wa Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO) kwenye ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam NA K-VIS BLOG/Khalfan Said MAAFISA wa polisi waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tatu ya polisi Wanawake kutoka Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika, (SARPCO), wamepata fursa ya kuelewa kwa undani huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mada mbalimbali zilizotolewa na Maafis wa Mfuko huo mwishoni mwa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Maafisa hao waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Kisayansi, (Forensic Bureau), ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi, (CP), Elice Mapunda walipata fursa ya kujua uendeshaji wa Mfuko huo ambao wanachama wake ni pamoja na Watumishi wote wa ...