Posts

CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI(MoCU) CHATOA ELIMU YA USHIRIKA KWA WAANDISHI WA HABARI.

Image
Makamu Mkuu wa Cho Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Prof,Faustine Bee akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja ya Elimu ya Ushirika kwa Waaandishi wa Habari wa mkoa wa Kilimanjaro. Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakishiriki warsha hiyo. Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ilitolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) katika Warsha ya siku moja iliyofanyika chuoni hapo. Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MoCU) Taaluma Dkt,Kitala Malamsha akizungumza wakati wa ukaribisho wa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya siku moja ya Elimu ya Ushirika kwa Waandishi wa Habari. Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakifuatilia mijadla katika warsha hiyo. Washiriki wa Warsha ya Elimu ya Ushiriki kwa Waandishi wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof ,Faustine Bee. Na ...

WANANCHI KATA YA MABILIONI WILAYANI SAME WATUMIA MAJI YENYE CHEMBECHEMBE ZA KINYESI CHA BINADAMU...

Image
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki akizungumza katika mkutano na wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same. Baadhi ya wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same wakimsikiliza mkuu wa wilaya alipozunumza nao katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya kata. Afisa Elimu wa Kata ya Mabilioni wilayani Same,Richard Sekibojo akimkabidhi taarifa ya kata hiyo Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za kata hiyo. Baadhi ya wananchi wa kata ya Mabilioni waliohudhuria mkutano huo. Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemarry Sitaki akifuatilia maelezo ya kero mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi katika mkutano huo.kushoto kwake ni Diwani wa kata ya Mabilioni, Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.. WANANCHI katika Kata ya Mabilioni wilayani Same wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutumia maji ya mto Ruvu yaliyopimwa na kugundulika kuwa na chembe chembe za Kinyesi cha...

KAMPUNI YA NETWORK LTD YAZINDUA DROO KUBWA YA MILIONI 60

Image
PICHANI:Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka, wakati wa uzinduzi wa mchezo huo wa kubahatisha nchini mapema jijini Dar es salaam (picha na ImmaMatukio Blog) Na Mwandishi Wetu Tatu Mzuka ni mchezo mpya wa jackpot uliobuniwa mahsusi kubadilisha maisha ya watu. Tatu Mzuka ni rahisi kucheza kwa kutumia simu ya mkononi, na kushinda ni baada ya kila lisaa limoja baada ya kucheza. Kucheza Tatu Mzuka unahitaji kuchagua namba zako tatu za bahati, kati ya 0 na 9 kwa kufanya muhamala kwenye simu ya mkononi, linganisha namba mbili ili kujiongezea nafasi ya kushinda mara mbili, au linganisha namba tatu na ushinde mara 200.

DAWASCO YAANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MFUMO MPYA WA UTOAJI NA UPATIKANAJI WA TAARIFA MUHIMU

Image
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya matumizi ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa vyombo vya Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi ili kutoa nafasi kwa wananchi kupata na kutoa taarifa sahihi za DAWASCO. Mmoja ya waendesha bodaboda akimuuliza swali Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWSCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa. Mwendesha bajaji akihojiwana ITV juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWASCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa. Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, ...

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YAWASOGEZA HUDUMA YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA NEWLAND WILAYANI MOSHI.

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Newland.  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa utamburisho wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo alipotembelea Mamlaka hiyo.  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) . Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa tanki la Maji linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland. Tenki la kuhifadhia Maji kwa ajili ya Mradi wa Maji yanayosambazwa katik...

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHANDISI RAMO MAKANI AKAGUA SHUGHULI ZA UTALII NA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

Image
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!.  Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia. Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza ma...